Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja, amekutwa leo
30/4/2014 akiwa amelala mtaroni maeneo ya Mitandi - Lindi Mjini. Mtu
huyo ambaye ilifahamika ana undugu na mtu mmoja aitwaye "BUSHIRI" katika
maeneo hayo alikutwa majira ya saa 2 asubuhi akiwa amelala usingizi
mzito mtaroni akionekana na michubuko kadhaa usoni. Mtu huyo ambaye
alinikwepa kumpiga Picha alinigomea nisimpige picha licha ya kumweleza
kuwa nahitaji kumsaidia kumpata mtu aliyemchukulia nguo zake. Mashahidi
wa tukio hilo walisimulia kuwa mtu huyo ambaye alioneka amelewa baada ya
kuamka, alikutwa akiwa amelala fofofo na baada ya kusikia sauti za watu
wakimshangaa ndipo alipozinduka na kujikuta YU UCHI na kuzuga kuwa
anatafuta msala wa kujisaidia. Mashahidi hao walisema hawajui zaidi ya
nini kilichompata usiku wa jana hali iliyomweka katika hali hiyo
"isiyoeleweka" kama ametendwa na wahuni ama amelipishwa pombe
aliyokunywa. Jamaa aliamua kujificha nyumani kwa Mudhihiri (jirani na
BOMOLEA) ili kukwepa asinaswe na Camera hii. Kwa kuwa hakutaka kusema
chochote na mhabarishaji nawasilisha kwenu tuzuie uhalifu wa aina hii
Mjini Lindi.
Picha na Lindi yetu Blog/ Blogs za Mikoa
Home »
» MAKUBWA: AKUTWA AMELALA MTALONI AKIWA HANA NGUO
0 comments:
Post a Comment