Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Uongozi wa Chama cha Wakulima (Taso) umekanusha madai
yanayotolewa na baadhi ya watu kuwa sherehe za wakulima na maonyesho ya
kilimo za Nanenane, hazitafanyika mkoani Lindi kama ilivyopangwa.
Tamko hilo lilitolewa na mwenyekiti wa Taso,
Engelbert Moyo wakati akizungumza na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya
sherehe hizo katika kikao kilichofanyika Lindi.
Mwenyekiti huyo alilazimika kukanusha madai hayo
kutokana na mjumbe mmoja kuomba uongozi utoe ufafanuzi kuhusu madai
yanayoendelea kutolewa na watu kupitia vyombo vya habari.
Mjumbe huyo alisema kuna madai kuwa sherehe hizo zitafanyika mkoa mwingine na si mkoa wa Lindi.
Akijibu hoja ya mjumbe huyo, Moyo alisema kuwa
madai hayo yapo huku akiwataka wanaoeneza uvumi kwa lengo la kuupotosha
umma kuacha kufanya hivyo mara moja.
Aidha moyo amewataka wananchi kutokubali kuyumbishwa na matamko yanayotolewa na baadhi ya watu,badala yake wajifunge kibwebwe
kuhakikisha Sherehe za maonesho ya nanenane
yanafanikiwa ipasavyo.Sherehe za sikukuu za wakulima na maonesho ya
Kilimo nanenane,kitaifa mwaka huu, yanafanyika mkoani hapa kwenyeviwanja
vya Ngongo ndani yaManispaa ya Lindi.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment