1
Wafanyakazi wa duka jipya la Tigo la Lindi Mjini katika nyuso za furaha na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda (aliyebeba mfuko wa Tigo) wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya iliyofanyika juzi.  
2
Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda (kushoto) akimsikiliza kwa makini Meneja wa duka jipya la Tigo lilipo Lindi Mjini Bw. Ahadi Mtweve (katikati) kuhusu huduma ya mauzo ya simu za kisasa pale alipofika kuzindua duka hilo juzi.  Duka hilo linalopatikana mtaa wa Makongoro nyuma ya stendi kuu ni duka la 41 la Tigo nchi nzima. 
3
 Meneja wa duka jipya la Tigo lililopo Lindi Mjini Bw. Ahadi Mtweve (katikati) akimuelezea Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda kuhusu huduma ya Tigo Pesa inayopatikana kwenye duka hilo mpya liliozinduliwa juzi na Mkurugenzi huyo. Kushoto ni mtoa huduma wa Tigo Pesa katika duka hilo Bi. Nasra Mbise. Duka hilo linalopatikana mtaa wa Makongoro nyuma ya stendi kuu ni duka la 41 la Tigo nchi nzima. 
4
Afisa wa Mahusiano kwa Wateja wa Tigo Bi. Pilila Kavishe (kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda (wapili kulia) katika picha ya pamoja na wateja wa Tigo waliozawadiwa kadi za vipaumbele kutoka kampuni hiyo ya simu. Kazi hizo zinampa uwezo mteja wa Tigo kupatiwa huduma za kipekee kama kutokukaa katika foleni anapofika katika duka la Tigo pamoja na kuondelewa kwa gharama mbali mbali anapohudumiwa katika maduka hayo.
Tigo imefungua duka jipya la huduma kwa wateja mjini Lindi ambayo itarahisisha upatikanaji wa huduma zake kwa wateja wa mjini hapo ambao awali walikuwa hawana namna ya kupata huduma za moja kwa moja kutoka kwenye kampuni hiyo ya simu.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi mjini, Kelvin Makonda, ambaye ameipongeza Tigo kwa hatua yake ya kuzidi kusogeza karibu huduma zake kwa watu wa Lindi.
“Pamoja na utatuzi wa kero za mawasiliano naamini ya kwamba duka hili jipya litakuwa kama kituo cha kutoa huduma mbali mbali ambazo wateja wenu wa Lindi watakuwa wanahitaji kutoka kwenu kila siku,” alisema Makonda.    
Makonda alisema kwamba huduma mbalimbali za mawasiliano zitolewazo na kampuni ya simu ya Tigo kama vile kupiga simu, kutuma SMS, mtandao wa Intaneti pamoja na huduma ya kutuma na kupokea fedha, zimekuwa kichocheo kikubwa katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. “Aidha huduma hizi zimeleta mageuzi chanya katika ufanyaji biashara na kuinua hali ya maisha ya maelfu ya wakazi wa Lindi na mamilioni ya watanzania kwa ujumla,” alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tigo wa kanda ya Pwani Bw. Brian Kalokola, amesema tawi hilo ambalo linalopatikana Lindi mjini mtaa wa Makongoro karibia na stendi kuu linatarajia kuwahudumia wateja wapatao 150 kwa siku kwa kuwapa huduma mbali mbali za Tigo zikiwemo huduma ya kuunganishiwa intaneti, usajili wa laini za simu, Tigo Pesa na huduma maalum za simu za kisasa (“Smartphones”).
“Duka hili lina manufaa makubwa kwa wateja kwa sababu limeleta huduma zetu karibu zaidi kwao. Pia linapatikana sehemu nzuri kibiashara kiasi kwamba litavutia hata wateja kutoka wilaya zingine na maeneo jirani kama Nachingwea, Liwale, Kilwa, Ruangwa na Lindi vijijini,” alisema Kalokola.
Duka hili linatoa huduma nyingine maalum zikiwemo uuzaji wa bidhaa mbali mbali kama simu za kisasa ambapo mteja anaruhusiwa kuzijaribisha kabla ya kununua. “Hii inamuwezesha mteja kufanya uamuzi sahihi katika kuchagua na kununua bidhaa inayokidhi mahitaji yake.”
Tawi la Lindi linafikisha jumla ya maduka yanayoendeshwa na kampuni ya Tigo nchini kufikia 41. Kwa mujibu wa Kalokola, kampuni hiyo ina mipango ya kufungua maduka mengine mengi zaidi katika sehemu mbali mbali nchini.