Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake mkoani Lindi, ambaye pia ni
Kamishna msaidizi wa Jeshi hilo,Acp Renatha Mzinga (kulia) akikabidhi sehemu
ya msaada wa vyakula kwa Muuguzi wa kambi ya wazee wasiojiweza ya
Rasibura,Manispaa ya Lindi,Bi,Elizabeth Njowele.
Kamishna msaidizi wa Jeshi la polisi Mkoani Lindi,Bi. Renatha Mzinga pamoja na
wanachama wa mtandao wa Polisi wanawake wakishiriki kazi ya usafi
katika kambi ya wazee na walemavu Mkoani Lindi.
Wana mtandao wa Polisi wakiendelea na zoezi la usafi.
Na Abdulaziz Video,Lindi
MTANDAO Wa Polisi Wanawake Mkoani Lindi (TPF-net) Umeipatia kambi ya
wazee wasiojiweza msaada wa bidhaa mbalimbali,zikiwemo nguo, vyakula
na mafuta wenye thamani ya Sh,309,500/-ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya siku 16 kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya mwanamke hapa nchini.
Akikabidhi msaada huo,mwenyekiti wa Mtandao huo na Ambae pia ni
kamishna msaidizi Polisi mkoani Lindi Acp Renatha Mzinga,alisema wao
wakiwa ni wanawake wa jeshi hilo,wameamua kuchanga kidogo walichonacho
kutoka sehemu ya posho zao,ili kuwakumbuka wenzao wanaokabiliwa na
matatizo mbalimbali ikiwemo wazee na walemavu wasiojiweza ikiwa katika
kuadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya mwanamke,
yaliyoanza Novemba 25 na kukamilika Decemba 10.
Acp Mzinga amesema iwapo wazee hao wangekuwa na viungo vyao kamili
pamoja na kuwa na maisha mazuri,wasingependa kubaki kuishi katika
kambi hiyo,huku wakisubiri kusaidiwa kutoka kwa watu wengine.
“Kama msingekuwa na ulemavu kama mlivyokuwa hivi sasa,msingekuwa na
sababu za kuishi katika mazingira ya aina hii hivyo sisi tumeona ni
bora tuje tuwafanyie Usafi wa makazi yenu na tuwapatie msaada mdogo
uliotokana na michango yetu..alisikika kamanda Mzinga wakati
akikabidhi misaada hiyo.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya wazee wenzake,mwenyekiti wa kambi
hiyo ya wazee,Mohamedi Chitawala,ameushukuru mtandao wa wanawake Jeshi
la Polisi mkoani hapa (TPF) kuweza kuwakumbuka watu walio na matatizo
mbalimbali yakiwemo ya viungo wanaoishi kwenye kambi hiyo,kwa
kuwapatia kile kidogo walichonacho.
Chitawala alisema kitendo cha Mtandao huo kuwasaidia wazee wa kambi
hiyo, sio ni furaha bali ni moja ya sehemu utekelezaji wa maagizo ya
mwenyezimugu wetu kupitia kwenye vitabu vyake anavyoutaka viumbe vyake
walio na uwezo kuwasaidia wenzao wasio na na uwezo wakiwemo wao
walemavu.
Katika kambi hiyo,iliyo chini ya kanisa katoriki Jimbo la
Lindi,imebaki na wazee walemavu wasiopungua saba (7) wakiwemo wanawake
watano na wanaume wawili,kati ya 15 waliokuwepo hapo awali,kufuatia
baadhi yao kufariki dunia na wengine kuamua kuondoka kambini
hapo,kutokana na kile kinachodaiwa huduma duni wanazozipata katika
kambi hiyo.
Chanzo;Michuzi blog
Chanzo;Michuzi blog
0 comments:
Post a Comment