WATOTO watatu wakazi wa Kijiji cha Likombora, Kata
ya Mihumo wilayani Liwale, Mkoa wa Lindi wamefariki dunia papo hapo baada ya
kulipukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa bomu.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Ephraem Mmbaga aliwataja
watoto waliofariki kuwa ni Seleman Namwera (13), Latifu Bayi (12) na mmoja
aliyefahamika kwa jina la Ponda (10).
Alisema kuwa Jumapili iliyopita mgambo wakiongozwa
na mshauri wao, Meja Tiba walifanya mazoezi ya kulenga shabaha ya silaha huko
kwenye Kijiji cha Kipule ambako mabomu matatu hayakulipuka na wakafanikiwa
kuyaokota mawili na kuyateketeza.
Kwa mujibu wa Mmbaga, siku ya tukio wanafunzi hao
wa Shule ya Msingi Likombora, walikwenda kucheza karibu na sehemu ya
kulengea shabaha ndipo walipoliokota hilo bomu na kuwalipukia.
Alisema kuwa mmoja wao alichanwachanwa kiasi cha
kutotambulika uso wake, na kwamba mabaki ya miili yao yalizikwa juzi.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment