Waziri wa nchi Ofisi ya Rais,mahusiano na uratibu,Stephen Wasira (aliesimama) akizungumza na watumishi mkoani Lindi,katika majumuisho ya ziara yake,iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi.
Na Abdulaziz Video,Lindi
WATUMISHI wa Serikali wakiwemo wataalamu mbalimbali,wametakiwa
kuwatumikia wananchi,wakiwemo wakulima wa zao la korosho kwa kuwawekea
Mfumo ambao utawapa Haki itokanayo na jasho lao.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais,mahusiano na uratibu,Stephen
Wasira,ametoa kauli hiyo,alipokuwa akizungumza na watumishi mkoani
Lindi,katika majumuisho ya ziara yake,iliyofanyika ukumbi wa
Halmashauri ya wilaya ya Lindi.
Akizungumza na watumishi hao,Wasira amesema Serikali inajipanga
kufanya marekebisho ya ununuzi wa zao la korosho kwa kutumia Mfumo wa
Stakabadhi mazao Ghalani,ili kumuwezesha mkulima kulipwa fedha kwa
lengo la kunufaika na Jasho lake.
Wasira amesema iwapo hakutakuwa na mfumo mzuri wa kuwatendea Haki
wakulima hao,ikiwemo kuwasimamia vizuri na kuwalipa fedha zao, itakuwa
ni vigumu kwao kuondokana na hali ya umasikini unaowakabiri hivi sasa
ndani ya Taifa lao.
Amesema iwapo watumishi ambao watashindwa kuwajibika ipasavyo kwenye
maeneo yao ya kazi,hakuna sababu ya kuwapandisha vyeo au kuendelea
kuwepo kazini.
“Hivi mtumishi mfano Afisa Kilimo ameshindwa kumbadilisha mkulima
kutoka kilimo cha kizamani na kwenda cha kisasa,kuna muhimu gani wa
kumpandisha cheo,,,,,,,,hapo asilalame kwa nini hajapandishwa Cheo
licha ya kuwepo kazini kwa muda mrefu,hapo anatakiwa aseme kwa nini
anaendelea kuwepo kazini bila ya kufukuzwa”Alisema Wasira.
Waziri huyo wan chi Ofisi ya Rais,Mahusiano na uratibu,amesema kamwe
umasikini wa wananchi wakiwemo na wakulima hautaweza kuondolewa kwa
utaraibu wa kuwaibia mazao yao,kwani kwa kufanya hivyo bado
wataendelea kujengewa mazingira magumu ya maisha yao
0 comments:
Post a Comment