Wazazi
mkoani Lindi wametakiwa kuwasomesha watoto wao ili kufuta ujinga na
kupunguza wimbi la vijana wanaokimbilia jijini DSM kufanya biashara
ndogondogo maarufu kama Machinga.
Wito huo umetolewa na
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Mh.Steven Wasira wakati wa
ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inafadhiliwa mfuko wa maendeleo ya jamii
TASAF Mkoani Lindi.
Akikagua ujenzi wa
maabara katika shule ya sekondari Mchinga waziri Wasira amesema maendeleo ya
nchi yanategemea wataalamu mbalimbali
wakiwemo wahandisi na
madaktari hivyo wazazi hawana budi kuwahimiza watoto wao kuchukua masomo ya
sayansi ili waweze kutumika katika kuendeleza rasilimali zilizomo.
Amefafanua kuwa wimbi la
uwekezaji linalotarajiwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara kufuatia uwepo wa gesi
katika eneo hilo na viwanda vinavyojengwa katika mikoa hiyo
kutahitaji wataalamu
waliosomea taaluma mbalimbali hivyo ujenzi wa maabara hiyo ifungue ukurasa mpya
wa vijana kujifunza masomo ya sayansi.
Kukamilika kwa ujenzi wa
maabara hiyo kunaibua changamoto nyingine ya upatikanaji wa vifaa vya
kufundishia ambapo Mkuu wa shule hiyo Mustapha
Nachuma
mafanikio ya kuongeza
wanasayansi katika shule hiyo huenda kusifanikiwe kutokana na gharama kubwa za
vifaa vya maabara.
Ujenzi wa maabara za
fizikia na baiolojia katika shule ya sekondari Mchinga II unatarajia kugharimu
Tsh.Mil. 92.6 hadi kukamilka utaongeza ufanisi katika mafunzo kwa vitendo
katika masomo ya sayansi.
0 comments:
Post a Comment