Idadi
kubwa ya wananchi katika wilaya ya Nachingwea Mkoa wa Lindi hawana
vyooambapo karibia nusu ya kaya zilizopo wilayani humo wahatumii vyoo bora.
Hayo yalibainishwa na Afisa afya na mazingira wa halmashauri
ya wilaya ya Nachingwea,Tumaini Kagina alipokuwa akiwasilisha mada kwenye
mafunzo kwa wajumbe wa kamati za afya za vijiji na wahudumu wa afya ya msing.
Amesema
kuwa Kati ya kaya 55083 zilizo kwenye wilaya hiyo ni kaya 25112 sawa na
asilimia 51 ndio zenye vyoo vyenye sifa huku wananchi wengi wakijisaidia
vichakani na kutaka jitihada za dhati za pamoja ili kufikia lengo la kuhakikisha
wananchi wanakuwa na vyoo bora.
Amesema kuwa hali hiyo imeonesha kuwa bado wana safari ndefu
ya kufikia lengo ka asilimia 80 ifikapo mwaka 2015 na hivyo amewasihi wananchi
kujenga makazi pamoja na vyoo bora.
Alibainisha kuwa kufuatia hali hiyo inaandaliwa kampeni ya
kitaifa ya usafi wa mazingira ambayo itasisitiza utupaji wa takataka,matumizi
ya vyoo bora na kunawa mikono wakati wote na hasa baada ya matumizi ya maliwato
ili kusaidia kupunguza hatari ya kupata maradhi ya mlipuko na maradhi mengine.
Amezitaja sifa za choo bora kuwa na pamoja
na kuwa na sehemu ya kunawia mikono iliyo na maji safi na ya kutosha katika
kibuyu chiriri na sabuni,chenye faragha ya kutosha na kujengwa kwa mali ghafi
za kudumu,kisichotoa harufu na kuchafua mazingira,kisicho hifadhi wadudu kama
nzi na kinachokubalika na jamii.
0 comments:
Post a Comment