Halmashauri
ya manispaa ya Lindi imeshindwa kukusanya ada za leseni za biashara kutokana na
kuchelewa kupata mwongozo kutoka serikali kuu na kusababisha kukosa mapato na
kushindwa kutekeleza miradi yake katika kipindi cha mwaka 2012/2013.
Hayo yamebainishwa na
mkurugenzi wa manispaa ya Lindi Kelvin Makonda katika kikao cha robo ya nne cha
baraza la madiwani ambapo amesema kwamba licha ya kukosa ada za leseni lakini
pia ilienda sanjari na kukosekana kwa malipo ya mnara wa zantel kutopatikana
katika kipindi chote cha mwaka.
Amesema
kuwa changamoto kubwa ilikuwa ni kuchelewa kwa ruzuku kutoka serikali kuu
kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoletwa mwishoni mwa robo ya
tatu na kusababisha kuchelewa kuanza utekelezwaji wa miradi ya maendeleo.
Hata
hivyo ametaja kuwa mradi wa kilimo cha umwagiliaji Ngongo, mradi wa maji
Kineng’ene, mradi wa ujenzi wa mabweni ya wavulana na wasichana sekondari ya Ng’apa na ujenzi wa madarasa
na maabara sekondari ya mingoyo kuwa imekamilika na mingine kufikia hatua za
mwishoni.
Pia amesema kuwa watu
wapatao 640 wamefanyiwa tathmini mashamba yao na kufanyiwa uthamini wa mali
katika kupisha upimaji wa viwanja katika eneo la Mmongo na Mabano kwa ushirikiano
baina ya halmashauri ya manispaa na taasisi ya dhamana ya taifa(UTT).
Amesema kuwa mradi
huo utawezasha manispaa kupata mapato kutokana na mauzo ya viwanja
vitakavyouzwa kwa wananchi kwa kugawana na UTT asilimia hamsini ya mapato.
0 comments:
Post a Comment