Na Thureya Dabas
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Bw. Ezekiah Oluoch
ameshangazwa na kitendo cha halmashauri ya lindi vijijini kukataa madai ya
walimu walioko Lindi.
Akizungumza na mwandishi kwa njia ya simu jana, Bw. Oluoch alisema kuwa kwa
taarifa walizonazo mpaka sasa ni walimu wa Lindi vijijini ambao wamekatwa madai
yao kutokana na sababu zisizojulikana.
"Sisi kama chama cha walimu hatua tuliochukuwa mpaka sasa ni kumuandikia
barua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lindi vijijini ili kujua chanzo cha walimu
hao kukatwa madai yao,"alisema.
Alisema kuwa amesikitishwa na hatua ya Mkurungezi huyo kukata madai ya walimu
kwa sababu zisizojulikana na kuongeza kuwa walimu walio wengi wanaishi kwenye
mazingira magumu kutokana na kipato duni.
Aidha alisema kuwa Mkurungenzi huyo alipaswa kuwa mstari wa mbele katika
kupigania madai ya walimu na sio kukata kwasababu wanategemea kuendesha maisha
na familia zao.
"Walimu wenyewe bado wana maslahi duni badala ya kupambana na kile kidogo
wanachopata, lakini utashangaa baadhi ya walimu wanakatwa madai yao pasipo
sababu zinazojulikana,"alisema.
Aliongeza kuwa wao kama CWT wanasubiri wapate majibu kutoka kwa Mkurugenzi huyo
ambapo pia wanahitaji awape majibu ikiwa ni pamoja na orodha ya majina ya
walimu hao na kiasi ambacho wamekatwa ili waweze kufuatilia kwa umakini zaidi.
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment