Mwandishi wetu, Liwale-Lindi
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Kapteni Honest Mwanossa, amewataka wananchi wa mkoa wa Lindi na Taifa kwa ujumla kutambua kuwa kuchangia mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya sio jambo la kisiasa.
Mwanossa aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya Nachingwea, kwenye makabidhiano ya mwenge wa uhuru yaliyofanywa kati ya wakuu wa wilaya za Nachingwea na Ruangwa mpakani mwa wilaya hizo hivi karibuni.
Kapten Mwanossa alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa katiba wakati utakapofika kwa ajili ya maendeleo yao na kusisitiza kuwa suala la katiba sio la kisiasa tena.
Alisema kuwa endapo wananchi watashiriki vema katika zoezi hilo ambalo ni muhimu litasaidia kuweka misingi ya utawala bora na kupunguza malalamiko yasiyokuwa ya msingi pamoja na migongano miongoni mwa jamii yetu.
Pia aliwataka pia wananchi wa mkoa huo kuchukia na kuikataa rushwa kwani imekuwa ni kikwazo katika kuleta maendeleo yao na kuichukia serikali iliyopo madarakani kwamba imekuwa ikiwakumbatia wala rushwa.
Kapteni Mwanossa amewataka pia watendaji wa serikali kuwa waadilifu na kuacha tabia ya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wateja ambao wanahitaji huduma kutoka kwao.
Alisema hali ya vitendo vya rushwa nchini imezidi kuwa mbaya kiasi kwamba wananchi wamekosa imani na viongozi wa serikali.
Kiongozi huyo akasema kutokana na kukosa kwa uwadilifu
huo kunawakatisha tamaa wananchi kujiingiza kwenye miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo ya Nachingwea, Rejina Chonjo alisema mwenge huo wa uhuru umezindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, afya na maghala yenye thamani ya sh.174, 830,450.
Mwisho.
Chanzo: Saidpowa
0 comments:
Post a Comment