Mkoa wa Lindi upo katika ukanda wa Pwani Kusini Mashariki mwa Tanzania na umepakana na Bahari ya Hindi upande wa Mashariki, mikoa ya Morogoro na Ruvuma upande wa Magharibi, mkoa wa Pwani upande wa Kaskazini na Kusini ni Mkoa wa Mtwara. Mkoa upo Kusini mwa Ikweta katri ya Latitude 7o55, na 10o longitude 36o55, na 40o Mashariki ya ‘Greenwich’. Mkoa huu ulizunduliwa rasmi mwaka 1971.
Mji wa Lindi ni mmojawapo ya Miji mikongwe nchini kwani ulianzishwa na wafanyabiashara wa kiarabu katika karne ya 11. Baadaye wakati wa ukoloni wa Kiingereza, wafanyabiashara Wahindi walihamia na kuweka makazi katika Mji wa Lindi.
Mji wa Lindi ulikuwa makao mkuu ya Jimbo la Kusini hadi mwaka 1952 wakati makao makuu yalipohamia Mtwara kutokana na sababu za kiuchumi na mazingira mazuri ya bandari ya Mtwara. Mabadiliko hayo yalisababisha Mji wa Lindi kudumaa licha ya kuwa makao makuu ya Mkoa wa Lindi kuanzia mwaka 1971.
Halmashauri ya Mji wa Lindi ilianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1953.
Eneo la Mkoa ni kilometa za mraba 67,000 na takriban robo ya eneo hili – sq.m 18,000 ni mbuga ya hifadhi ya wanyama ya SELOUS GAME RESERVE. Kati ya eneo hilo lote la Mkoa ni Ha. 5,250,000 ndizo hufaa kwa kilimo na ni asilimia 10 tu ya eneo hilo hadi sasa linatumika
Source: Tanzania Regions Site
0 comments:
Post a Comment