Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na.WAMJW,Ruangwa.
Wizara
ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto inatarajia kutoa
mwongozo wa utoaji tiba kwenye hospitali zote nchini ili kuwe na mfumo
mzuri wa dawa muhimu ili kuepusha madaktari kuagiza dawa ambazo zipo nje
ya mfumo wa dawa muhimu.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ziara
yake ya kuangalia hali ya upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea
huduma za afya vya Serikali .
“Kabla
ya mwisho wa mwaka tunataka kutoa muongozo huo(Standard Treatment
Guidline) kwa sababu imekua changamoto kwani wale wauzaji wakubwa wa
dawa wamekua wakizitembelea hospitali kubwa na kuwarubuni wanunue dawa
zao ambazo zipo nje ya dawa zetu muhimu”
Kwahiyo
muongozo huo itakua kila ugonjwa dawa ya kwanza itakua ipi na kama
itashindika dawa itakayofuata dawa ipo na hizo dawa zitaagizwa na
kutunzwa na Bohari ya Dawa(MSD).
Hata
hivyo Dkt.Ndugulile amewataka watendaji wa hospitali hiyo kuweka
utaratibu na mpangilio mzuri na unaohitajikwa wa utunzaji wa dawa kwenye
stoo ya madawa iliyopo hospitalini hapo,baada ya kukuta hakuna upangaji
mzuri wa dawa na vifaa tiba “mmenithibitishia kwamba dawa zote
mnazipata kwa asilimia 90 hivyo ni vyema Mfamasia wa Wilaya kuzipanga
dawa hizo vizuri na kuweka kiyoyozi ambacho kitasaidia kutunza dawa kwa
muda bila kuharibika”
Alisema
hivi sasa nchi haina tatizo la upatikanaji wa dawa kwani bajeti ya dawa
hivi sasa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 30 mpaka zaidi ya bilioni
260 kwa mwaka huu wa fedha “bajeti hii imekua ikitolewa na Mhe.Rais
amekua akizitoa fedha zote,hivyo hatuna shida ya fedha hivyo nasi
hatutarajii kuwa na shida ya dawa na dawa tunazokuwa tunazipata zitunzwe
vizuri”.
Aidha,amezitaka
kamati za afya katika ngazi za zahanati,vituo vya afya na hospitali
zinafanya kazi ipasavyo kwa kusimamia matumizi mazuri ya dawa.
Kwa
upande wa ubora wa huduma za afya kwa vituo vya kutolea huduma za afya
vya serikali hivyo kumekua na mkakati wa kuwa na ubora wa vituo vya
serikali kwa kuwapatia nyota kulingana na ubora uliopo kwenye vituo kwa
kuangalia utoaji wa huduma,maabara na sehemu zingine za kutolea huduma.
Kwa
upande wa Mfuko wa afya wa jamii(CHF) Dkt.Ndugulile amewapongeza wilaya
hiyo kwa kusajili kaya 13,788 kutoka 978 mwaka 2016/2017,ambapo
wamewapatia vitambulishovya matibabu wazee 4,000.“hivi sasa Serikali
inataka kuwa na bima kwa wote kwani gharama ya matibabu kwa sasa ni
kubwa sana hasa na kumekua na ongezeko la magonjwa yasiyo ya
kuambukizwa,hivyo tunataka kuwasaidia wananchi ambao hawawezi kumudu
gharama hizo ili anavyokwenda kwenye vituo vyetu asiwaze masuala ya
kutoa fedha”alisema Dkt.Ndugulile.
Akisoma
ripoti ya Wilaya hiyo Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Ernest
Ntahuka Alisema Halmashauri hiyo imeweza kuboresha hali ya upatikanaji
wa dawa kwa asilimia 85 kutoka asilimia 60 ya mwaka 2015/2016.Hata hivyo
alisema Halmshauri ya Ruangwa kwa mwaka 2017/2017 imetenga shilingi
milioni 650 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya na tayari
imeshatenga eneo la ujenzi lenye ukubwa wa hekari 60 ambapo ramani ya
ujenzi huo tayari imeandaliwa
0 comments:
Post a Comment