Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof Dos Santos Silayo akiwa kwenye mkutano na watendaji wake wa Kanda ya Kusini (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuwataka meneja kuchukukua hatua kwa watendaji wasio waadilifu mapema hivi leo.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Kusini Ebrantino Mgiye (mwenye koti jeusi) akiwasolisha mafanikio na changamoto zinazoikabili kanda huku akifuatiliwa kwa umakini na Meneja Msaidizi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu Bw. Gaudence Kilasi (aliyekaa) mapema hivi leo.
Baadhi ya Watendaji wa TFS Kanda ya Kusini wakichukua kumbukumbu katika Kikao cha Wafanyakazi kilichoendeshwa na Mtendaji Mkuu wa TFS Prof Dos Santos Silayo kuanza kuzungumza nao mapema hivi leo hii.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof Dos Santos Silayo akimfuatilia kwa umakini Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Kusini Ebrantino Mgiye (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mafanikio na changamoto ya miaka mitatu ya kanda hiyo mapema hivi leo.
Na Tulizo Kilaga Lindi
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof Dos Santos
Silayo amewataka meneja wa misitu nchini kusita kuchukua hatua pale
wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watendaji wanaojihusisha na vitendo vya
rushwa kwenye vituo vya ukaguzi wa mazao ya misitu.
Ametoa
agizo hilo leo tarehe 04/10/2017, alipotembelea na kuzungumza na
wafanyakazi wa TFS Kanda ya Kusini katika ofisi za Wilaya ya Lindi ya
Taasisi hiyo.
“Kuna
tuhuma za hovyo nimesikia, watu wanakamatwa na mazao ya misitu
yaliyovunwa ama kusafirishwa kinyume na sheria, wanaombwa kitu kidogo na
baadhi ya watumishi wasio waaminifu ili kuhalalisha mizigo hiyo na
wakigoma, mizigo yao hukamatwa, nataka kuwaona mnachukua hatua
stahiki,”amesema.
Mtendaji
Mkuu ameeleza kuwa licha ya TFS kuwa na changamoto nyingi anaimani na
taasisi hiyo na amewataka watendaji wake kufanya kazi kwa kushirikiana
na kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya na kuzingatia weledi,
uzalendo na uadilifu, akiahidi Serikali kufanyia kazi changamoto
zinazowakabili.
Awali,
Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Kusini Ebrantino
Mgiye alisema miongoni mwa changamoto zinazokabili taasisi hiyo ni
pamoja na uhaba wa watendaji.
Hata
hivyo, Mtendaji Mkuu amewataka watendaji wa TFS kujikita katika
utendaji wa kimkakati ili kuboresha usimamizi na uhifadhi wa raslimali
za misitu na Nyuki kwa ajili ya kuchangia katika mahitaji ya kijamii,
kiuchumi, ki-ikolojia, na ki-utamaduni kwa kizazi cha sasa na kijacho.
0 comments:
Post a Comment