Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb)
alipotembelea banda la JKT kujionea namna ya uzalishaji mali unaofanywa na Jeshi hilo wakati wa uzinduzi
wa
 maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika 
viwanja vya maonesho ya kilimo wa Ngongo Mkoa wa lindi, jana tarehe 
1/8/2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb) (kulia) akizungumza jambo na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew J. Mtigumwe wakati wa uzinduzi wa
maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja
 vya maonesho ya kilimo wa Ngongo Mkoa wa lindi, jana tarehe 1/8/2017.
Na Mathias Canal, Lindi 
Naibu
 Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. Wiliam Tate Ole Nasha (Mb) 
amesema kuwa kwa muda mrefu serikali imekuwa ikipata malalamiko kutoka 
kwa wananchi mbalimbali hususani kwa wakulima
nchini Tanzania wakipinga kodi na tozo mbalimbali zinazotozwa kwani 
zimekuwa zikiwanyonya badala ya kuwakwamua na wimbi kubwa la umasikini.
Ameyasema
 hayo jana tarehe 01/08/2017 wakati akizungumza na wakulima wadau wa 
kilimo Mifugo na Uvuvi na wananchi kwa ujumla wakati wa uzinduzi wa 
sikukuu ya wakulima – nane nane, Maonesho yenye
kauli mbiu ya “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” yanayofanyika
Kitaifa kwenye uwanja wa maonesho ya kilimo wa Ngongo Mkoani Lindi.
Alisema
 kuwa kutokana na malalamiko hayo Rais wa Jamhuri ya muungano wa 
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliamua kufuta baadhi ya kodi na 
tozo katika sekta ndogondogo za mazao ili
kuibua tija ya uwajibikaji na ukuzaji wa uchumi.
Alisema Jumla ya tozo 80 kati ya tozo 139 zimefutwa na tozo nne (4) zimepunguzwa viwango. Tozo, kodi na ada zinajumuisha 
kufutwa kwa tozo kumi (10) na mbili (2) kupunguza viwango kwenye zao la tumbaku.  Kwenye
zao la kahawa zimefutwa tozo 17 na moja (1) kupunguzwa kiwango; sukari 
zimefutwa 16; pamba tozo zilizofutwa ni mbili (2); kwenye korosho tozo 
mbili zimefutwa na chai imefutwa tozo moja (1).
Katika kuongeza upatikanaji wa pembejeo tozo tatu (3) zimefutwa na moja (1) imepunguzwa kiwango kwenye mbolea na 
tozo saba (7) zilizokuwa kwenye mbegu nazo zimefutwa. Katika Ushirika jumla ya tozo 20 zimefutwa katika ngazi mbalimbali.
Alisema kuwa katika
 Mifugo; kodi, ada na tozo saba (7) ambazo zilikuwa
kero kwa Wafugaji, Wafanyabiashara na Wawekezaji nazo zilifutwa na 
kubakiza zile tu zenye uhusiano wa moja kwa moja katika uendelezaji wa 
Sekta ya Mifugo. Tozo zilizofutwa zinajumuisha mbili (2) kwenye maziwa; 
nyama tozo nne (4) na moja (1) kwenye afya ya mifugo.  
Katika
 Uvuvi, jumla ya kodi, ada na tozo tano (5) ambazo ni kero kwa Wavuvi, 
Wafugaji wa viumbe kwenye maji na wawekezaji nazo zimefutwa. 
Alisema
 kuwa Serikali itaendelea kuchambua kwa kina tozo, ushuru na ada 
mbalimbali zilizobaki katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa lengo la 
kuangalia uhalali wa kuwepo kwake
ili kuwapunguzia wakulima, wafugaji na wavuvi mzigo wa tozo, ushuru na 
ada zisizokuwa na tija.
‘‘Serikali pia imechukua hatua za makusudi kupunguza ushuru wa mazao uliokuwa unatozwa na Serikali za mitaa kutoka asilimia 5
hadi asilimia 3  kwa
 mazao ya biashara na kufikia asilimia 2 kwa mazao ya chakula. Vile 
vile, Serikali imezielekeza Serikali za Mitaa kuacha kutoza
ushuru kwa wazao yanayosafirishwa halmashauri moja kwenda Halmashauri 
nyingine yenye uzito usiozidi tani moja (1)’’ Alisema Mhe Nasha
Aliongeza
 kuwa Hatua nyingine iliyochukuliwa ni ya kusamehe kodi ya ongezeko la 
thamani kwenye vyakula vya mifugo vinavyotengenezwa hapa nchini ili 
kupunguza gharama ya
kununua chakula hicho kwa Wafugaji. Serikali pia, imesamehe kodi ya 
ongezeko la thamani kwenye mayai ya kutotoleshea vifaranga, lengo likiwa
 ni kupunguza gharama ya uzalishaji vifaranga na kukuza Sekta ndogo ya 
Ufugaji ili iweze kuongeza mchango katika Pato
la Taifa.
Mhe Nasha alisema kuwa Kuanzia msimu huu wa kilimo Wakulima wa korosho
watapata bure pembejeo aina ya salfa zilizokuwa zikiuzwa kwa bei ya ruzuku. 
Hatua hiyo ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ni  kuhakikisha
kuwa vikwazo vyote vilivyokuwa vinawakabili wakulima wa zao la korosho vinaondolewa ili waongeze uzalishaji na tija zaidi kutokana na zao hilo. 
Aidha
 alisema kuwa Serikali itaendelea kuhimiza matumizi ya Mfumo wa 
Stakabadhi Ghalani. Mfumo huu umesaidia kupanda kwa bei ya korosho na 
mapato kwa wakulima kupitia vyama vikuu vya
ushirika vya TANECU, MAMCU, RUNALI, Lindi Mwambao, TAMCU na CORECU.  
Alisema
 wakulima na wafanyabiashara Wote ni mashahidi kuwa katika msimu wa 
ununuzi uliopita wa mwaka 2016/2017 vyama hivyo viliuza korosho na 
kuwalipa wakulima jumla ya Shilingi bilioni
809.18 ikilinganishwa na malipo ya Shilingi bilioni 293.09 msimu wa 
2015/2016. Kiasi hiki cha fedha ni kikubwa na ni mafanikio makubwa 
ambayo ni ya kujivunia.
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment