Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb)
akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tizeba wakati wa uzinduzi wa
maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya
maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, jana tarehe 1/8/2017. (Picha zote na Mathias
Canal)
Na Mathias Canal, Lindi
Serikali
imeongeza uzalishaji katika mazao makuu ya chakula hususani mahindi,
mchele, mtama, uwele, na mikunde jambo linalopelekea kujitosheleza kwa
chakula kwa wastani wa asilimia 100.
Aidha, Uzalishaji mwingine umeongezeka kwenye mazao ya jamii ya mizizi kama muhogo, ndizi, viazi vitamu na mviringo.
Hayo
yamesemwa jana tarehe 01/08/2017 na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Wiliam Tate Ole Nasha (Mb) wakati akizungumza na wakulima
wadau wa kilimo Mifugo na Uvuvi na wananchi kwa
ujumla wakati wa uzinduzi wa sikukuu ya wakulima – nane nane, Maonesho
yenye kauli mbiu ya “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati”
yanayofanyika Kitaifa kwenye uwanja wa maonesho ya kilimo wa Ngongo Mkoani Lindi.
Alisema
kuwa Katika mwaka 2015/2016 Sekta ya Kilimo ilichangia asilimia 29.1 ya
Pato la Taifa ikilinganishwa na asilimia 29.0 mwaka 2014/2015. Mchango
mkubwa katika Pato la Taifa ulitokana na
Sekta ya Kilimo, ikifuatiwa na Sekta nyingine za kiuchumi.
Mchango
huo mkubwa ni Kwa kuwa asilimia kubwa ya Watanzania wanashiriki katika
shughuli za kilimo, hivyo kilimo kinachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza
kipato na kupunguza umaskini.
Mhe
Nasha Alisema kuwa uzalishaji wa mazao, mifugo na uvuvi umeimarisha
zaidi usalama wa chakula na lishe nchini, ambapo katika mwaka 2015/2016
uzalishaji wa chakula ulikuwa ni tani milioni 16.2
ikiwa ni ongezeko la tani milioni 0.7 (sawa na 4.5%) ikilinganishwa na
tani milioni 15.5 mwaka 2014/2015.
Uzalishaji
wa mazao ya nafaka umeongezeka kutoka tani milioni 8.9 mwaka 2014/ 2015
hadi tani milioni 9.5 mwaka 2015/ 2016 ikiwa ni ongezeko la tani
milioni 0.6 (sawa na 6.7%). Uzalishaji wa
mahindi umeongezeka kutoka tani milioni 5.9 mwaka 2014/2015 hadi tani
milioni 6.1 mwaka 2015/2016 sawa na ongezeko la tani milioni 0.2 (sawa
na 3.4%). Uzalishaji wa mchele uliongezeka kutoka tani milioni 1.9 mwaka
2014/ 2015 hadi tani milioni 2.2 mwaka 2016
sawa na ongezeko la tani milioni 0.3 (sawa na 15.8%).
Vilevile,
uzalishaji wa mazao ya chakula yasiyo nafaka umeongezeka hadi kufikia
tani milioni 6.7 ikilinganishwa na tani milioni 6.6 kwa mwaka 2014/ 2015
ikiwa ni sawa na ongezeko la tani milioni
0.1 (sawa na 1.5%).
Kwa
ujumla uzalishaji wa mazao ya chakula ukilinganishwa na mahitaji ya
tani milioni 13.2 ya chakula na matumizi mengineyo katika mwaka
2016/2017 unaonesha kuwepo kwa ziada ya tani milioni 3.0
za chakula. Kutokana na hali hiyo Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa
asilimia 123 ambayo ni ongezeko la asilimia 3 ikilinganishwa na asilimia
120 ya mwaka 2015.
Katika
mwaka 2016/2017 idadi ya mifugo nchini imefikia ng’ombe milioni 28.44,
mbuzi milioni 16.67 na kondoo milioni 5.01. Pia, wapo kuku wa asili
milioni 37.43, kuku wa kisasa milioni 34.5, nguruwe
milioni 1.85 na punda wapatao 572,357. jumla ya mitamba 634 ilizalishwa
kutoka mashamba ya Serikali na Kampuni ya Ranchi za Taifa - NARCO
ikilinganishwa na mitamba 646 iliyozalishwa mwaka 2015/2016. Aidha,
jumla ya mitamba 10,820 ilizalishwa na Sekta binafsi
na kusambazwa kwa wafugaji wadogo nchini ikilinganishwa na mitamba
10,803 iliyozalishwa mwaka 2015/2016.
Mhe
Nasha alisema kuwa Vituo vya Kanda vimeendelea kuimarishwa kwa kupatiwa
vitendeakazi, ukarabati wa miundombinu na mitambo ili kuhakikisha
upatikanaji wa huduma ya uhimilishaji wakati wote.
Jumla
ya dozi 100,000 za mbegu bora za mifugo zilizalishwa ikilinganishwa na
dozi 80,000 mwaka 2015/2016. Pia, ng’ombe waliohimilishwa wameongezeka
kutoka 221,390 mwaka 2015/2016 hadi ng’ombe
457,557 mwaka 2016/2017.
0 comments:
Post a Comment