Home » » SHEHENA NYINGINE VIROBA YANASWA

SHEHENA NYINGINE VIROBA YANASWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Said Hamdani

JESHI la Polisi mkoani humu, limekamata mamia ya katoni za viroba kufuatia msako unaoendelea kufanywa na jeshi hilo.

Kamanda wa Polisi mkoani humu, Renatha Mzinga, alisema msako huo uliondeshwa juzi katika wilaya tatu kati ya tano za Mkoa wa
Lindi na kufanikisha kukamatwa kwa katoni 956 za viroba pamoja na lita 62 za pombe aina ya gongo.

Kamanda Mzinga alisema watu sita wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo na wanaendelea kuhojiwa polisi huku watatu kati yao wakiwa ni wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwa kufuata sheria.
Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Nelson Fidelis (23) na Ludovick Mshumbusi, ambao ni wafanyabiashara wa Mji Mdogo wa Masoko wilayani Kilwa ambao wanatuhumiwa kukutwa na katoni 62 na Sinza Classic, anayedaiwa kukutwa na katoni 894 za Konyagi, Vodka,Valuer, Zanzi, Boss na Bismark ambayo zilizofungashiwa kwenye vifungashio vilivyokatazwa na serikali.
Wengine waliokamatwa na lita 62 za gongo ni Peter Nazarius (45), Rukia Mtenekea (30) na Mohamed Amour, wakazi wa wilayani Ruangwa.
Hali kadhalika, Kamanda Mzinga alisema msako huo pia uliwezesha kukamatwa kwa mitambo mitatu ya kutengenezea gongo.
Kamanda Mzinga alizitaja aina ya pombe zilizokamatwa kuwa ni Konyagi, Vodka, Valuer, Zanzi, Boss, Bismark na gongo.

Alisema watuhumiwa wote hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili baada ya kukamilika upelelezi.
Aidha, Kamanda Mzinga ametoa wito kwa watu wenye pombe za aina hiyo kuzisalimisha polisi.
CHANZO GAZETI LA NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa