Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Adili Mhina, Lindi.
Kaimu
Katibu Mtendaji, Wizara ya Fedha na Mipango upande wa Tume ya Mipango,
Bibi Florence Mwanri amefanya ziara katika eneo lililotengwa kwa ajili
ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata Gesi Asilia lililopo katika mtaa wa
Likong’o Manispaa ya Lindi na kushauri uongozi wa Manispaa hiyo kuongeza
juhudi za kuhakikisha wananchi waliopisha mradi huo wanalipwa fidia kwa wakati.
Mwanri alieleza kuwa ni vyema uongozi ukatilia mkazo umuhimu wa kuwalipa fidia wananchi ili waweze kujiletea maendeleo yao kwa kuwa hawawezi tena kuendelea kutumia eneo hilo.
Alieleza
kuwa dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda inaenda sambamba
na kuwajali wananchi wake kwa kutoa fidia kwa mujibu kanuni na sheria pale wanapolazimika kuachia maeneo yao ili kupisha miradi ya maendeleo.
Mwanri
aliongeza kuwa pamoja na kuwa mradi huo utakapojengwa na kukamilika
utakuwa na faida kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla utasaidia pia kuinua
kipato kwa wanachi wa Lindi kutokana na fursa mbalimbali za ajira
zitakazojitokeza kwa wakazi hao.
Nae
Mtendaji wa Mtaa wa Ling’oko ambapo ndipo mradi huo unapotekelezwa, Bw.
Jacob Anton alieleza kuwa wananchi wa eneo hilo wana matarajio makubwa
na wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali kwa kuwa wanaamini ujio
wa kiwanda hicho utasaidia kuboresha maisha yao.
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi kutoka Tume ya Mipango ikiongozwa na Naibu Katibu
Mtendaji huyo, kwa sasa inaendelea na zoezi la ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara ambapo itatembelea
miradi ya Serikali na ile ya sekta binafsi kwa lengo la kuhakikisha
malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21)
yanatekelezwa kwa ufasaha.
0 comments:
Post a Comment