Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi
*Msako wa DC kupita Jan. 15 mwakani
*Asiye na choo kutozwa faini ya sh. 50,000
MKUU
WA MKOA wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ametoa wiki mbili kwa wakazi wa
jimbo la Ruangwa kuhakikisha kuwa wanajenga vyoo ili kujiepusha na
ugonjwa wa kipindupindu.
Amemtaka
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Joseph Mkirikiti afanye msako wa nyumba
kwa nyumba ifikapo Januari 15, 2017 na endapo atakuta kuna mkazi wa
kijiji chochote hajajenga choo, basi atozwe faisi ya sh. 50,000 mara
moja.
Ametoa
leo (Jumatano, Desemba 28, 2016) wakati akizungumza na wananchi wa
vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi
na Chibula wilayani humo ambako alikuwa akiwasalimia wananchi kabla ya
kumkaribisha Waziri Mkuu azungumze na wakazi wa vijiji hivyo.
Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na ameamua kutumia muda huo kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo.
Mkuu
huyo wa Mkoa amesema wakulima wengi wamevuna korosho msimu na baadhi
yao wamelipwa vizuri, hivyo hawana budi kutumia sehemu ya fedha hizo
kujenga vyoo ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko na hasa kipindupindu.
“Hili ni agizo la Serikali siyo yangu binafsi kwa hiyo ni amri halali. Kikilipuka
kipindupindu, naanza na Mkuu wa Wilaya kabla na mimi sijaulizwa na
Mheshimiwa Waziri Mkuu au Mheshimiwa Rais,” amesema.
Katika hatua nyingine, Bw.
Zambi amewahimiza wakazi wa vijiji hivyo wapande miche ya mikorosho
katika msimu huu wa kilimo pindi mvua zitakapoanza kwani iliyopo imekaa
kwa zaidi ya miaka 50 na sasa haizai matunda ya kutosha.
“Mkoa
wetu una mpango wa kubadilisha miti ya mikorosho kwani mingi ni ya
zamani na imelkaa kwa zaidi ya miaka 40 hadi 50 na hivi sasa haina tija
kwenye mazao yake. Mti mzuri wa korosho unazaa hadi kilo 40 lakini hii
iliyopo sasa hivi inatoa kilo 10 tu,” amesema.
Amesema
Serikali imeagiza kila kijiji kiandae miche 5,000 kwa mwaka na kuwapa
wananchi kwa bei nafuu na mpango huo tumeshaanza kuutekeleza.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, DESEMBA 28, 201
0 comments:
Post a Comment