Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kushoto Meneja Uhusiano wa Airtel bw Jackson Mmbando akielezea huduma zitakazotolewa na mnara wa Airtel uliojengwa kijiji cha Cheleweni kwa Mkuu wa wilaya Lindi bw, Shaibu Ndemanga (wapili kulia) mara baada ya kuzindua mnara huo huku wananchi wakisikiliza. katikati ni Meneja wa Airtel Lindi by Saleh safy. Airtel imejenga mnara huo kutoa mawasiliano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo Safy. Airtel imezindua huduma hiyo ili kuboresha , huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na kuwaweza wananchi wa Lindi kupata mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii
Mkuu wa Wilaya Lindi bw, Shaibu Ndemanga akiongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa mnara wa Airtel utakaotoa mawasiiano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo. anaefuata ni diwani wa viti maalum Lindi Bi, Somoe Pamui na Meneja Mauzo wa Airtek Bw, saleh Safy. Airtel imezindua huduma hiyo ili kuboresha , huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na kuwaweza wananchi wa Lindi kupata mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii
Mtandao wa Airtel kutumika kuhimiza elimu ili wazazi kuandikisha watoto Lindi vijijini
katika
juhudu za kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia maeneo ya
pembezoni mwa nchi, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua
mnara wake wa mawalisiliano na kuanzisha hduma za simu kwa mara ya
kwanza katika kijiji cha cheleweni mkoa wa Lindi.
Huduma
hizi mpya za mawasiliano zitawafikia wakazia wa vijiji vya Ng’apa
ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo
yanayowazunguka vijiji hivyo kwa kuwahakikishia wakazi wote wa Lindi
vijijini huduma za mawasiliano za uhakika, huduma za kifedha kwa njia ya
mtandao Airtel Money na hatimae kuendesha shughuli zao za kila siku
kiuchumi na kijamii
Akiongea
wakati wa uzinduzi, Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga alisema “
tunayofuraha kupata huduma za mawasilino hapa cheleweni na vijiji vya
jirani. Airtel kwa kuzindua mnara huu, serikali tunaungano jitiada hizi
za kuboresha mawasiliano huku vijiji kwa sasa wakazi wa vijiji hivi
mtaweza kutumia huduma ya mawasiliano kwa kufany a biashara zenu za nazi
kwa kujitafutia masoko sehemu nyingine lakini pia itasaidia kuondoa
tatizo lakutembe na fedha nyingi pale mnapofanya biashara kwa kuwa
mtatumia huduma za kifedha za Airtel Money kujichukulia fedha zenu
wakati wowote
Mkuu
wa wilaya aliongeza kwa kusema “Mawasiliano haya yatasaidia sana wilaya
yangu katika kukuza elimu kwa kuwa nitaweza kuwawasiliana na watendaji
wangu wote wakati wowote. Sasa nitoe tamko kwamba nimeongea na Airtel
ili kutuma ujumbe wa meseji kwa wazazi wote kwa kuwa ndio mtandao
unaotumika na wengi hapa katika vijiji vyetu vya ng’apa ng’apa kuhusu
kuandikisha watoto wote waliomaliza shule za msingi waende sekondari,
Airtel wamenikubalia sasa ikiwa mzazi atakaidi kuitikia wito
nitamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfunga”.
Nataka
kuona huduma hii ya Mtandao wa Airtel tunayoizindua leo inaleta tija
katika shughuli za uchumi kama vile uzalishaji wa korosho, kusaidia
biashara ndogo za kati na kubadilisha maisha ya jamii kwa ujumla.
Napenda kuchukua fursa hii kuwahasa wakazi pia kuilinda miundombinu ya
mawasiliano haya ili yaduma. Alimalizia kusema Mh, Ndemanga
Kwa
upande wake Meneja Mauzo wa Airtel, Saleh Saphy “Tunayofuraha kutoa
huduma za uhakika na gharama nafuu nchi nzima, kwa wakazi wa Lindi ,
tunawahakikishia ofa kabambe za msimu huu wa sikukuu kupitia ofa yetu
maalumu ya “Wadatishe” ambayo mnaweza kupata simu orijino kwa gharama
nafuu hadi ya shilingi 79,000 tu.-. vilevile wateja wanaweza kupata
vifurushi vya intaneti vya 1G kwa shilingi 1000 wakati huu wa msimu wa
sikukuu .
Kupitia
huduma ya mawasiliano wateja wataunganishwa na huduma za intaneti,
huduma za kifedha za Airtel Money kutuma na kupokea pesa, kupiga simu
wakati wowote, kusajili simu zao na pia kupata nafasi ya kusoma masomo
ya ufundi ya VETA kupitia simu zao. Hizi ni baadhi tu za huduma zetu
hivyo natoa wito kwa wakazi wa cheleweni, Ng’apa na Michee kujiunga na
timu ya Airtel SIBANDUKI na kufurahis huduma zetu.” Alisisitiza Saphy
0 comments:
Post a Comment