Na Abushehe Nondo,Maelezo.
ASILIMIA 80 ya
Watanzania wamesema juhudi za maendeleo hazina budi kupewa kipaumbele baada ya
uchaguzi na kukataa mikutano ya kisiasa ambayo wanadai hukwamisha shughuli za maendeleo.
Taarifa ya utafiti
huo iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaaam na Shirika la Utafiti la TWAWEZA
ilisema kuwa utafiti huo umebeba maoni ya wananchi kuhusu demokrasia, udikteta na maandamano nchini
Tanzania.
Aidha taarifa hiyo
iliongeza kuwa takwimu za muhtasari huo
zinatokana na na utafiti wa sauti za wananchi ikiwa ni moja ya programu
za Twaweza.
Pia katika utafiti
huo, wataalamu hao waliweza kubaini kuwa asilimia 49 ya wananchi wanakubaliana
na kuzuiwa kwa mikutano ya vyama vya siasa kutokana na kwamba huvuruga umakini
wa Serikali na Wananchi.
Katika suala la
kumhusisha Rais Maguli na udikteta utafiti huo umebaini kuwa asilimia 58 ya
Watanzania wanapinga uwepo wa udikteta katika serikali ya awamu ya Tano ya Rais
John Magufuli.
Aidha utafiti huo wa
Twaweza pia umebainisha kuwa asilimia 50 ya wananchi wamesema hakuna uwezekano
wa wao kushiriki kwenye maandamano yoyote.
Kuhusu uamuzi wa Rais
Magufuli kuzuia mikutano ya hadhara utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 60
wanamuunga mkono Rais katika kuzuia mikutano ya hadhara ya kisiasa.
Utafiti huo wa
Twaweza umekuja baada ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe
Magufuli kujipatia pongezi nyingi kwa jitihada zake za kupambana na na vitendo
vya rushwa.
0 comments:
Post a Comment