Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi 
CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa watu kweny mkutano wa 
kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa shule ya msingi Mpili pili mkoani Lindi,
Katika
 mkutano huo wa hadhara Dkt.John Pombe Magufuli amesema kuwa Serikali 
atakayounda baada ya kuchaguliwa na Watanzania Oktoba 25 mwaka huu, 
itahakikisha inawatumikia huku akiweka wazi kuwa yeye  hakuwa na mchezo 
kwani dhamira yake ni kutatua shida za wananchi kwa spidi kubwa.
Amesema
 anatambua shida ambazo watanzania zinawakabili na hivyo uamuzi wake wa 
kuomba nafasi hiyo ni kuhakikisha anakabiliana nazo huku akisisitiza 
serikali yake,Mawaziri atakaoteua wajiandae kufanya kazi na atakayeona 
hawezi ni bora akajiweka pembeni mapema kabla ya kuapishwa ama akakataa 
uteuzi.
Dkt Magufuli pia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya wali0jinyakulia
 tuzo hizo usiku wa kuamkia leo huko Dallas, Marekani ambapo Diamond 
alichukua tuzo tatu katika vipengele vya Best Dance Video kupitia wimbo 
wake wa Nana, Best Male East Africa Artist na Artist of The Year huku 
wimbo wa Alive alioshirikiana na Brackets ukichukua tuzo ya Best 
Inspirational Song of The Year.
Wakati
 huohuo mwanadada, Vanessa Mdee akichukua tuzo ya Best Female East 
Africa huku Ommy Dimpoz akichukua tuzo ya Best New Comer na kufanya 
Tanzania kukusanya jumla ya tuzo tano.
Dkt
 Magufuli amefanya kampeni zake katika jimbo la Nachingwea,Ruangwa,jimbo
 la Mtama na Lindi mjini huku akisimamishwa na wanachi mara kadhaa kila 
alikokuwa anapita.
Sehemu
 ya umati wa kazi wa mji wa Lindi Mjini wakishangilia wakati Mgombea 
Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura ya
 kuwania nafasi ya Urais.PICHA NA MICHUZI JR-LINDI
Mjumbe
 wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete akimuombea kura za kutosha
 mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni 
uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mpili pili mkoani Lindi 
jioni ya leo.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia mkutano wa kampeni a Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli mjini Lindi.
Mgombea
 Urais wa CCM Dkt Magufuli akimuombea kura kwa wananchi Mgombea Ubunge 
wa jimbo la Mtama,Ndugu Nape Nnauye kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea
 Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.
Mjumbea
 wa kamati ya ushindi ya kampeni za Mgombea Urais wa CCM,Mh Bernad Membe
 akiwahutubia wananchi wa Lindi mjini kwenye mkutano wa kampeni wa 
Mgombea Urais wa CCM zilizofanyika katika uwanja wa shule ya msingi 
mpili pili,mkoani Lindi.
Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi 
mgombea Ubunge wa jimbo la Ruangwa,Mh.Kassim Majaliwa,kwenye mkutano wa 
kampeni uliofanyika leo mchana mjini Ruangwa mkoani Lindi mara bada ya 
kumkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM.
Mmoja 
wa wafuasi wa chama cha CHADEMA akizungumza mbele ya umati mkubwa wa 
wakazi wa mji wa Ruangwa mara baada ya kurejesha kadi ya chama chake kwa
 Mgombea Urasi wa CCM Dkt Magufuli,ambapo wanachama wapatao 150 wa vyama
 mbalimbali pinzani walirejsha kadi zao.
Wananchi
 wa jimbo la Mtama wakishangilia jambo wakato mgombea Urais wa CCM Dkt 
John Pombe Magufuli alipokuwa akizimwaga sera zake za kuomba nafasi ya 
kuwania Urais wa awamu ya tano ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa
 mwaka huu utakaohusisha nafasi ya Urais,Wabunge na Madiwani.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa jimbo la Mtama,mkoani Lindi kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi
 wa jimbo la Mtama wakifuatilia sera za mgombea wa Urais wa CCM Dkt Jonh
 Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema loe mchana kwenye mkutano 
wa kampeni.
Wananchi wa jimbo la Mtama wakifuatila mkutano kampeni wa mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.
Wananchi
 wa jimbo la Mtama wakishangilia jambo wakato mgombea Urais wa CCM Dkt 
John Pombe Magufuli alipokuwa akizimwaga sera zake za kuomba nafasi ya 
kuwania Urais wa awamu ya tano ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa
 mwaka huu utakaohusisha nafasi ya Urais,Wabunge na Madiwani.
Mgombea
 Ubunge wa jimbo la Mtamba,Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa 
jimbo hilo wakati wa kumuombea kura mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe 
Magufuli,ili aibuke mshindi na kuiongoza Tanzania katika awamu ya 
tano,kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.
Wakazi
 wa mji wa Lindi mjini wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa shule ya 
msingi Mpili pili wakisubiri kumsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt 
Magufuli,
Mgombea
 Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la 
Mtama,Ndugu Nape Nnauye wakifuatilia jambo,kwenye mkutano wa kampeni 
uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingin Mpili pili,Lindi mjini.
Baadhi ya Wananchi wa Mjini Lindi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea Urais Dkt John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti
 wa CCM Mkoa wa Lindi,Mzee Ali Mtoba akizungumza jambo wakati wa 
kumkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,ahutubie wananchi na 
kumwaga sera zake ikiwemo na kuwaomba kura wakazi wa Lindi,za kuwania 
nafasi ya Urais katika uwamu ya tano,kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa 
kufanyika Oktoka 25 mwaka huu.
Wakazi
 wa mji wa Lindi mjini wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa shule ya 
msingi Mpili pili wakisubiri kumsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt 
Magufuli,
Wakazi
 wa mji wa Lindi mjini wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa shule ya 
msingi Mpili pili wakisubiri kumsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt 
Magufuli,
Mgombea
 Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya Wananchi 
waliokuwa wemefunga barabara wakati akitokea wilaya ya Nachingwea 
kuelekea wilaya ya Ruangwa kuwahuubia wananchi kwenye mkutano wa 
kampeni 
Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi 
mgombea Ubunge wa jimbo la Ruangwa,Mh.Kassim Majaliwa,kwenye mkutano wa 
kampeni uliofanyika leo mchana mjini Ruangwa mkoani Lindi.
 























 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment