Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Lindi
kumekucha, pilikapilika za maandalizi ya Maonyesho ya Nane Nane kitaifa
mwaka huu zimepamba moto ambapo Mgeni Rasmi katika maonesho hayo
yatakayofunguliwa Jumatatu Agosti 3, 2015 anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda. Maonyesho hayo ya
mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague
Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”.
Mratibu
wa Maonyesho ya Nane Nane kutoka wilaya ya Newala Ado Kiwangu
akiwaonesha na kuwaeleza wageni waliotembelea bustani ya michungwa juu
ya namna bora ya kuzalisha machungwa ikiwa ni pamoja na matumizi ya
mbolea ya samadi inayoipa michungwa virutubishi stahiki, hivyo michungwa
huzaa sana.
Mfugaji
wa sungura Ahmed Juma Ntava akiwalisha sungura wakati wa maandalizi ya
Maonyesho ya Nane Nane kitaifa mkoani Lindi mwaka huu ambapo Mgeni Rasmi
katika maonesho hayo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda yatakayofunguliwa Jumatatu Agosti 3,
2015.
Mmoja wa watumishi wa Jeshi la Magereza nchini akivuna kabichi iliyokomaa tayari kwa matumizi ya mboga.
Afande
Majid Nyange kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akieleza namna ya
kutumia mazingira ya asili kutengeneza jokofu yenye gharama nafuu kwa
kutumia mkaa, miti, sakafu na nailoni yeusi kwa ajili ya kusharabu
mwanga.
Maeneo
mbalimbali ya bustani na mifugo yaliyoandaliwa tayari kwa maonesho Nane
Nane kitaifa mkoani Lindi mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu “Matokeo
Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na
Ufugaji”(Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Lindi).
0 comments:
Post a Comment