Home » » Liwale washauriwa kujiunga na Vicoba

Liwale washauriwa kujiunga na Vicoba

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Wajasiriamali Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi wameaswa kujiunga na Vicoba na kujenga tabia ya kutunza akiba ili kufikia malengo waliojiwekea.
Ushauri huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila alipotembelea vikundi vya vikoba na wajasiriamali hao.
Mwananzila alisema msingi wa ujasiriamali na vikoba ni akiba, ili biashara iweze kuleta tija lazima uwapo utaratibu wa kujiwekea akiba mara kwa mara. Aliwataka kujinga na Vicoba ili kukabiliana na umaskini nchini.
Chanzo;mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa