Waziri
Mkuu Mizengo Pinda na msafara wake wakiangalia eneo utakapochimbwa mtaro wa
kupitishia bomba la gesi.
Mafundi
wakiendelea na kazi ya kuunganisha mabomba kabla ya kuyalaza na kuyafukia chini
kwenye mitaro.
Mkuu
wa mkoa wa Lindi akiwa na Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili mkoani humo na
kuendelea na ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha MEIS Merea Barabuu akimkaribisha Waziri Mkuu
Mizengo Pinda katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo eneo la
Machole Mkoani Lindi.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi na wafanyakazi wa ujenzi kiwanda cha
MEIS faida zitzkazotokana na kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa
gasi kijijini hapo kwa njia rahisi baada ya kuunganishwa kutoka bomba kuu la
gasi ikiwemo ajira kwa wanachi na upatikanaji wa saruji kwa bei nafuu ili
kuboresha makazi yao.
Baadhi
ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha MEIS
kilichopo eneo la Machole Mkoani Lindi.
Picha
ya sura na muonekano wa kiwanda cha MEIS kitakapokamilioka. (Picha
zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO-Mtwara).
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na mafundi wanaojenga bomba la mradi wa gasi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua mradi huo.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akieleza hatua iliyofikiwa katika ujennzi wa bomba la gasi linalojengwa kutoka Mtwara hadi Dar es salaam kwa Waziri Mkuu na msafara wake. Kushoto ni Balozi wa China nchini, Lu Younqing.
Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akimsikiliza Waziri wa Nishati na Prof. Madini Sospeter Muhongo akizungumzia ujenzi wa bomba la gasi eneo la Bungu mkoa wa Pwani.
======== ======== =========
Na
Eleuteri Mangi-Maelezo Mtwara.
Waziri
Mkuu amewaasa wanachi kutunza miundo mbinu ya mradi wa gasi nchini.
SERIKALI
imewapa jukumu wananchi wanaoishi maeneo linapopita bomba la kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi
Dar es Salaam la kulitunza na kulilinda kwa
manufaa yao na taifa zima.
Wito
huo ulitolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo
Pinda leo alipokuwa katika ziara ya
kikazi kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba hilo. Waziri
Mkuu Pinda alisema Serikali inavihakikishia vijiji lilipopita bomba hilo kuwa
watapatiwa umeme unaotokana na uzalishaji wa gasi na utakuwa wa gharama nafuu.
Zaidi
ya hayo, gasi itatumika kwa matumizi ya nyumbani kwa kuunganishiwa bomba la
gasi na ambao hawatafanikiwa watakuwa na fursa ya kupata mitungi ya gesi ambayo
itakuwa ya bei nafuu. Waziri
Mkuu ameagiza mashirika ya Shirika la gasi na Petroli Tanzania (TPDC) na Mradi
wa Nishati Vijijini (REA) wachukue jukumu la kuboresha maisha ya wananchi wa
maeneo lilipopita bomba hilo katika maeneo ya barabara, shule, kuwapatia maji
safi na salama,kuwaboreshea utoaji wa huduma za afya kwa kuboresha zahanati na
vituo vya afya kama mchango wao kwa jamii.
Kwa
upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alisema kuwa
serikali kupitia shirika la TPDC na REA itahakikisha wanachi waishio vjijini
wanapata umeme mapema iwezekanavyo.
Kwa
kuthibitisha kauli hiyo Prof. Muhongo alisema serikali kupitia TPDC na REA
imetenga sh. Bilioni 20 kwa awamu ya kwanza ambayo itasimamiwa na REA wakati
awamu ya pili nayo itatumia bilioni 20 iotkaysimamiwa na TPDC.
Katika
ziara hiyo Waziri Mkuu aliambatana na mke wake bi Tunu Pinda, Balozi wa China
nchini, Lu Younqing, Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, mbunge
wa Mchinga Said Matanda na Fatma Mikidadi mbunge wa viti maalum. Maeneo
aliyotembelea Waziri Mkuu ni pamoja na Vikindu, Jopika, Bungu, Ikwiriri,
Somanga, Somanga Fungu, Kitomanga na Lindi.
0 comments:
Post a Comment