Madiwani 14 kati ya 25 wa Manispaa ya Lindi wamejiorodhesha na
kuandika barua kwa Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo kumtaka kuitisha
kikao maalum cha Baraza la madiwani ili kupata taarifa mbalimbali
ikiwemo hatua ya Mkuu wa Mkoa kufunga Ofisi ya Mipango Miji kwa zaidi
ya mwezi mmojapamoja na kuanza kwa mauzo ya Viwanja huku madiwani
wakiwa hawana taarifa.
Hatua hiyo ya madiwani hao akiwemo Mbunge wa jimbo la Lindi Mjini Bw
Salum Barwany imekuja kufuatia kutoshirikishwa kwa madiwani kuhusiana
mambo mbalimbali yanayotekelezwa hususan Ulipaji wa Fidia na mauzo ya
viwanja chini ya mpango wa UTT pamoja na hatma ya mgogoro wa wananchi
wenye maeneo hayo yaliyoanza kuuzwa.
Akiongea na waandishi wa Habari,Diwani wa kata ya Nachingwea ,Omary
Chitanda alieleza kushangazwa na hatua ya mkuu wa mkoa kufunga ofisi
ya Idara ya Mipango Miji kwa zaidi ya mwezi mmoja kinyume na taratibu
za ofisi za serikali.
“Sisi ndio Halmashauri ila imetushangaza sana Kitendo cha mkuu wa mkoa
kufunga ofisi ya mipango miji na kuunda tume ambayo ilimaliza kazi ila
sisi madiwani tumeomba taarifa ya Tume hiyo atupewi akaunda tume tena
kuhusiana na mgogoro wa wananchi na manispaa kuhusiana na ardhi
iliyochukuliwa katika mpango wa UTT Pia madiwani atupewi taarifa Je
sisi kweli ni wawakilishi wa wananchi tunafichwa hivi?alielezaChitanda
Pamoja na hilo Madiwani hao walieleza kusikitishwa na kutofahamishwa
na hatma ya Vibanda 8 vilivyojengwa katika eneo la kituo cha mabasi
na baadhi ya madiwani kinyume na utaratibu na kuzuiwa na manispaa hiyo
kwa muda mrefu.
Jitihada za kumpata mkuu wa mkoa Lindi,Ludovick Mwananzila ana kwa
ana hazikuzaa matunda na kufanikiwa kumpata kwa njia ya Simu ambapo
alikiri na kueleza kuwa tayari ameshatoa maelekezo kwa Meya na
Mkurugenzi wa manispaa kwa utekelezaji na pia Taarifa ya Tume zake
amewasilisha Tamisemi na kwa kwa Waziri Mkuu.
Hivi karibuni Ofisi ya Manispaa ya Lindi imeanza kutangaza kupitia
vyombo vya habari kuhusiana na Uuzaji wa Viwanja katika maeneo ya
mmongo,Mabano na Mitwero chini ya mpango uliofadhiliwa na UTT
Madiwani waliojiorodhesha na barua yao Ni kama inavyosomeka na sahihi zao
Baadhi ya madiwani waliokutana na waandishi wa Habari kutoa
tamko la kumtaka Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Lindi kuitisha kikao
maalum ndani ya siku 14 ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya madai ya
madiwani.
Meya wa Manispaa ya Lindi
Barua iliyoandikwa na Madiwani hao kwenda kwa Meya.
0 comments:
Post a Comment