HALMASHAURI
ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, imeingia mkataba na nchi za Ulaya,
ikiwemo Serikali ya Ufaransa wa kusimamia, kutunza na kuendeleza
rasilimali za urithi yakiwemo mambo ya kale yaliyopo katika wilaya hiyo.
Zoezi
la kutiliana saini juu ya mkataba huo, ulioongozwa na Balozi wa nchi
hizo ,Filberto Sebregodi, limefanyika Ukumbi wa Jengo la PEC uliopo mji
mdogo wa Masoko.
Hayo yameelezwa na Balozi wa wanchi hizo za umoja
wa Ulaya Filiberto Sebregodi, alipokuwa akizungumza katika mkutano
uliowakutanisha wadau wa masuala ya utalii wilayani Kilwa.
Mkataba
huo wa miaka mitatu, una lengo la kuendeleza masuala ya mambo ya kale
(Utalii) unahusisha masuala ya usimamizi na utunzaji wa mambo ya Kale,
yakiwemo magofu misikiti na nyumba zilizopo visiwa vya Songo Mnara na
Kilwa kisiwani.
Akizungumza kabla ya kutiliana saini kwa mkataba huo
,Balozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya, Filiberto Sebregondi, alisema nchi
hizo zimeamua kushirikiana na Halmashauri hiyo, kutangaza rasilimali za
Urithi zilizopo katika wilaya hiyo, ili kukuza maendeleo ya kiuchumi na
kijamii ndani ya wilaya hiyo.
Balozi huyo amesema Kilwa ni wilaya
iliyo na vivutio vya kila aina vya utalii, ambavyo kama vitatunzwa na
kutangazwa vitaweza kukuza utalii wake wa ndani na kuongeza uchumi kwa
wananchi wake na serikali kwa ujumla.
Alisema kufuatia kuwepo kwa
vivutio hivyo, ndipo Ubalozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya na Serikali ya
Ufaransa ikaamua kusaini mkataba wa miaka mitatu na Halmashauri ya
wilaya hiyo ya Kilwa katika kutunza, kusimamia na kuendeleza rasilimali
za urithi zilizopo wilayani.
" Kilwa ni wilaya tajiri kwani ina
rasilimali nzuri tu, hususan zile zakiutalii, lakini hazifahamiki
kutokana na kutotangazwa,"alisema Balozi Filiberto Sebregodi.
Naye,
mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Mohamedi Ally Mtopa,
akitoa shukrani zake kwa niaba ya wananchi wa wilaya, ameishukuru nchi
za Ulaya kwa kutupatia mradi huo, kwani utaendelea kuimarisha rasilimali
za mambo ya kale.
Mtopa akasema bado Kilwa itaendelea kudumisha
uhusiano wa kirafiki kati yake na nchi hizo za Ulaya ikiwemo ya
Ufaransa, kwani yapo mambo mengi wanayoyahitaji kutoka katika nchi hizo.
Mradi huo wa miaka mitatu na utaenda sanjari na kubadilishana
uzoefu kwa sababu rasilimali za urithi zilizopo Ufaransa ambazo
zinawaingizia fedha na kukuza uchumi kwa wananchi wa wilaya hiyo ya
Kilwa
Chanzo;Majina
0 comments:
Post a Comment