Home » » Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi ajiuzulu

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi ajiuzulu

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi, Ally Chitanda, ametangaza kujiondoa katika nafasi hiyo akieleza kuchoshwa na uamuzi wa kikanda na kikabila unaoendelea ndani ya chama hicho.
Mbali na Uenyekiti, Chitanda  pia alikuwa  Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa na Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu- Sekretarieti nafasi ambayo pia alitangaza kujiuzulu jana, lakini akaahidi kuendelea kuwa mwanchama mwaminifu wa Chadema.
Hata hivyo katika maelezo yake ya sababu za kujiuzulu alisema: “Sioni sababu ya kuendelea kuwa mwana Chadema, sioni sababu ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi.”
“Sioni sababu ya kuwa kiongozi kwa kuwa kipaumbele cha Chadema ni kukijenga chama Kaskazini, basi sisi wa Lindi tunawatakia kila la heri….”
Alisema amefikia hatua hiyo baada ya uamuzi wa Kamati Kuu ya Chama hicho, kuwavua nyadhifa Zitto na mwenzake Dk Kitila Mkumbo wiki iliyopita.
Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa kuhusu uamuzi huo wa Chitanda alisema kuwa hawezi kumzunguzia kwa kuwa ni mtu mdogo katika chama akitaka atafutwe msemaji wa Chadema Tumaini Makene aliyesema: “Mwambieni Chitanda atoe barua ya uteuzi wake.”
Chaanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa