Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono  wanafuzi wa  Chuo 
cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA) , Lindi kabla ya kuzindua 
mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana mkoani Lindi.Kulia 
ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah  Moshi na  wa pili 
Kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila na kushoto wa 
kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Nassoro  Hamidi.
  Mwanafunzi wa  wa  Chuo cha  Mafunzo ya  Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA), Lindi akimwonesha    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  kifaa cha kukata vyuma   katika karakana ya uungaji  vyuma.
 Mwanafunzi
 wa  wa  Chuo cha  Mafunzo ya  Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), Lindi 
akimwonesha    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  kifaa cha  ufundi wa 
magari katika karakana ya ufundi wa magari.
  Mama Salma Kikwete , akipata maelekezo kutoka kwa mwanafunzi wa Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA), Edwin  Nduguru(kushoto)
 jinsi deep stick inavyofanya kazi ya kupima kiwango cha oil kilichopo 
katika injini ya gari alipotembelea karakana ya ufundi wa magari wa chuo
 hicho jana. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah  Moshi (kulia) , Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Nassoro  Hamidi (kushoto).
 Mama Salma Kikwete  (aliyevaa kitenge ) akiongea jambo  na  Meneja wa  British  Gas Tanzania ambao ndiyo wafadhili  wa mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli, Kate Sullam (kushoto) jana  kwenye   Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA) , Lindi .Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi.
 
 Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete  akikata utepe  ikiwa ni ishara 
kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana  kwenye Chuo
 cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA)  Lindi . Kulia ni  
Mkurugenzi Mkuu wa VETA,  Mhandisi Zebadiah  Moshi na Kushoto wa tatu  
ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila, kushoto ni Afisa 
Uhusiano wa chuo hicho Dora Tesha.
 
 Mama Salma Kikwete  akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mradi wa 
mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana  kwenye Chuo cha  Mafunzo ya 
Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA)  Lindi . Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA,
 Mhandisi Zebadiah  Moshi na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, 
Ludovick   Mwananzila.
 Picha
 ya pamoja  na baadhi ya viongozi   na wanafunzi  wa  Chuo cha  Mafunzo 
ya Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), Lindi. Picha na Anna Nkinda-Maelezo
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment