Home » » Avunjika miguu akipandisha bendera

Avunjika miguu akipandisha bendera



Akizungumza akiwa kitanda namba 4 katika wodi namba nne ya majeruhi ya wanaume katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine alisema 

MKAZI wa Mtaa wa Mwenge Manispaa ya Lindi, Abdulahmadi Rashid amenusurika kufa baada ya kuanguka kutoka mwenye mlingoti wa kupeperushia bendera na kuvunjika miguu yote wakati alipokuwa anafunga bendera ya Chama cha Wananchi (CUF).

Tukio hilo lilitokea saa 12:00 asubuhi siku ya Desemba 9, mwaka huu katika Tawi la CUF lililopo Kituo cha Mabasi ya mkoa katika Manispaa ya Lindi.Akizungumza akiwa kitanda namba 4 katika wodi namba nne ya majeruhi ya wanaume katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine alisema anamshukuru Mungu kwa kumnusuru na kifo kwani hakutegemea kama atakuwa salama kutokana na ajali hiyo.
Alisema kuwa mlingoti alikuwa amepanda una urefu wa zaidi ya futi 18 na kwamba alikuwa anakwenda kubadilisha bendera ya chama chake ambayo ilikuwa imechakaa kwa kuwa ilikuwa ya muda mrefu.

Alisema wakati akifunga bendera hiyo ghafla mlingoti huo ulikatika katikati na kumsababishia kuanguka na kupoteza fahamu huku akiwa amevunjika katikati ya vifundo vya miguu yake yote miwili.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa CUF mkoa wa Lindi ambaye ni mbuge wa Jimbo la hilo Salamu Baruani alikiri kuwapo kwa tukio na kueleza kuwa chama kinamuhudumia kwa kumpatia mahitaji yote tangu akutwe na tatizo hilo.

Baruani alisema kuwa wamelipokea tatizo hilo kama la chama kwa kuwa kijana huyo ni miongoni mwa wananacha ambao wanakitumikia chama kwa vitendo bila ya kujali hali ya kiuchumi ya chama.

Aliwaomba wanachama wengi ne kumsaidia kijana kwa kutoa kila walichonacho ili apate na atibiwe ili aweze kuruhusiwa akaendelee na kazi za chama

MWANACHI

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa