Home » » WATANZANIA TUONYESHE MOYO WA HURUMA TUMSAIDIE HUYU MAMA.

WATANZANIA TUONYESHE MOYO WA HURUMA TUMSAIDIE HUYU MAMA.


Mkazi wa Kijiji cha Mnamba kata ya Nampa mkoa wa Lindi, Rafael Mohamed  (36) anayesumbuliwa na uvimbe wa pua tangu mwaka 1984 akisaidiwa na mtoto wake  Shafi Abdalah mwenye umri wa miaka 18 kwenda kutafuta mahitaji ya kila siku ,mama huyo anaomba msaada wa matibabu kwani madaktari wa Hospitali ya mkoa wa Lindi wameshindwa kumfanyia upasuaji.
NANI HAPA WA KUMSAIDIA MWINGINE: Mwanafunzi wa shule ya msingi Nyagao ya wasioona na wanaoona, iliyopo Wilaya ya Lindi,  Hussein Omari   akimsikiliza   Rafael Mohamed, anayesumbuliwa na  ugonjwa wa uvimbe ambao umemfanya ashindwe kuona wakati  walipokwenda shuleni hapo kwa ajili ya kupatiwa msaada wa  vyakula mbalimbali vilivyotolewa msaada na wasamaria wema.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa