Mtoto Sofia Hamis mwenye umri wa miaka 12 anayesoma darasa la pili katika shule ya Msingi Litehu wilayani Tandahimba,Mkoani Mtwara ambaye alitoweka mwanzoni mwa MWEZI huu,amepatika akiwa katika shimo lililo katika msitu wa kijiji cha Mmeda wilayani humo huku akiwa hai baada ya jitihada zilizofanywa na Mganga wa kienyeji kutoka kijiji cha Mtama Lindi Vijijini.
Mtoto huyo alitoweka nyumbani kwa Mama yakeMzazi tarehe 08/05/2012 akitokea shuleni na toka siku hiyo hakukuwa na taarifa za kuonekana kwake na jitihada mbalimbali za kumpata mtoto huyo kutozaa matunda
huku siku zikisonga mbele.
Kufuatia kupotea kwa mtoto huyo kulizaa taharuki mbalimbali kijijini hapo hali iliyomfanya mama mzazi kuhangaika kutafuta kwa njia ya imani za jadi na kufanikiwa kujuzwa na mganga alietambulika kwa jina la Rukia Akili Salum mkazi wa Mihogoni-Mtama Lindi Vijijii kuwa mtoto yupo hai na anao uwezo wa kumtoa katika mazingira aliyokuwepo.
Mama wa Mtoto huyo alifanikiwa kusafirisha mganga huyo hadi kijiji cha MMEDA -kilichopo kata ya LITEHU Tandahimba ambapo baada ya kufanya shughuli zake alifanikiwa kwa pamoja kumkuta mtoto huyo akiwa shimoni akiwa hawezi kuongea vizuri huku mwili ukitawaliwa na upele.
Baada ya kufanikiwa kumpata mganga huyo alisafiri nae kwenda Mtama kwenye makazi yake ili ampatie tiba ambazo hadi Mimi namfikia mtoto huyo alikuwa tayari amerudi katika hali yake ya kawaida
0 comments:
Post a Comment