Home » » WATU SABA WAKIWEMO ASKARI POLISI WAKAMATWA LINDI KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA RAIA WA PAKSTANI

WATU SABA WAKIWEMO ASKARI POLISI WAKAMATWA LINDI KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA RAIA WA PAKSTANI


watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi

WATU saba wakiwemo askari Polisi watano na raia wawili wamefikishwa
katika mahakama ya mkoa wa Lindi, wakikabiliwa na mashitaka
mawili,likiwemo dai la kusaidia usafirishaji wa watu 13 wenye asili ya
Pakstani mwishoni wiki iliyopita.


Mwandishi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Lindi Abdulaziz Video anaripoti kuwa ,Watuhumiwa hao wamefikishwa Leo, mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo,
Aluu Nzowa na kusomewa kosa lao na wakili wa Serikali, Mwahija Hamadi.


Waliofikishwa mahakamani hapo ni,ASP Alphonce Magabe, E 5754 Coplo
Hilari,F 6069 D/c Francis, G2334 Pc James,PC Joseph, wote ni askari wa
kituo cha Lindi mjini,Kasimu Mussa na Emmanuel Joseph,madereva na na
wakazi wa Jiji la Dar es salaam.


Akiwasomea makosa yao katika kesi hiyo namba 44/2012,mwanasheria wa
Serikali, Mwahija Hamadi,amedai mahakamani hapo kuwa mei 03 mwaka
huu,usiku washitakiwa wote kwa pamoja walisaidia kusafirisha raia hao
wenye asili ya Pakistani.
Katika Shitaka la pili,linalowakabiri washitakiwa wa kwanza hadi wa
watano,mwanasheria huyo wa Serikali alidai mahakamani hapo kuwa ni
uzembe wa kushindwa kutekeleza majukumu yao, huku wakijua fika ni
waajiriwa wa Jeshi la Polisi.


Raia hao wa kipakistani walikuwa wakisafiri kutoka jijini Dar es
salaam, kuelekea nchi jirani za Msumbiji na Afrika ya kusini,
wakitumia usafiri wa basi ndogo Toyota Coaster yenye namba za usajili
T 368 BPW iliyokuwa ikiendeshwa na mshitakiwa Kassimu Musa.


Mwanasheria huyo wa Serikali aliiambia mahakama hiyo kwamba
washitakiwa wote kwa pamoja wamefanya makosa chini ya vifungu vya
Sheria namba 5/2008 kifungu kidogo cha 1 na 2 na Sheria namba 148
chini ya Sheria ya uzuiaji usafirishaji binaadamu.


Washitakiwa wote kwa pamoja wamekana makosa yote waliyokuwa
wamesomewa na kupelekwa rumande, kesi yao itatajwa tena mei 15 mwaka
huu


.Aidha, mwanasheria huyo aliiambia mahakama hiyo kwamba chini ya
Sheria kifungu namba 6/2008 Shitaka la aina hii mara nyingi halina
dhamana.


Kauli hiyo ya mwanasheria ilipingwa vikali na washitakiwa hao,huku
wakiiomba mahakama iwape Stahiki kwani Shauri lao,halihusu mauaji wala
ujambazi hivyo kuwanyima dhamana ni kuwanyima Haki zao za msingi.


“Mh, Hakimu tunaomba mahakama itupe Stahiki kwani sisi sio
majambazi,kwani kuna watu wameshawahi kushitakiwa kwa mauwaji,lakini
wanapewa dhamana inakuwaje sisi tusipewe dhamana kwa hili”Alidai
mshitakiwa wa kwanza ASP Alphonce Magabe.


Aidha,baada ya Hakimu Nzowa kusikiliza kwa pande zote mbili,ameamua
kutoa uwmuzi huo wa kuwapa dhamana au la mei 15 mwaka huu, hali
iliyowafanya washitakiwa wote kupelekwa rumande.


Baada ya matamshi hayo na Hakimu Nzowa kutelemka kutoka kwenye kiti
chake,mke wa mshitakiwa wa kwanza ASP Magabe, aliongoza msafara wa
vilio,uliochangia kundi la maaskari waliofurika mahakamani wakiwemo
polisi na washitakiwa wenyewe kushindwa kujizuia na kuangusha vilio,
huku mke wa askari huyo akipewa msaada wa kutoka nje na watumishi wa
kike wa mahakamani hapo.


Katika kile kinachoonekana wasipigwe picha na waandishi wa Habari
waliokuwepo mahakamani hapo,washitakiwa wote saba walipitishwa mlango
mwingine badala ya ule wa kawaida na kusafirishwa kupelekwa rumande na
gari aina ya Land Cruser yenye namba za usajili STK 3941 inayotumiwa
na mwanasheria wa serikali. alieongoza kesi hiyo
Mwisho.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa