Home » » wakuu wapya wa wilaya mkoani Lindi wala viapo

wakuu wapya wa wilaya mkoani Lindi wala viapo

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mh Abdallah Hamisi Ulega

 Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dkt, Nassoro Ally Hamidi akila kiapo
Mkuu wa Wilaya ya  Ruangwa Mh Agnes Elias Hokororo  akipokea nyenzo za kufanyia kazi
  Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mh  Regina Reginal Chonjo akila kiapo
MKUU wa mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila amewataka wakuu wa wilaya mkoani humo, kufanya kazi waliyokabidhiwa ikiwemo kuwatumikia wananchi katika maeneo yao kwa kufuata kanunu na maadili kwa kushirikiana na jamii ili kuwaletea maendeleo kutokana na hali duni za wananchi wa mkoa wa Lindi wenye raslimali nyingi.
Wito huo umetolewa na Muda mfupi baada ya kuapishwa wakuu wapya wa wilaya za mkoa wa Lindi ambapo aliwahimiza kufuata kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali zilizowekwa na Serikali, kwani ndio misingi mikuu

itakayowasaidia kutekeleza vema majukumu yao ya kila siku katika wilaya zao.


Aidha alisisitiza wakuu hao kusimamia na kufuatilia miradi inayotekelezwa katika wilaya zao,pamoja na kuzingatia fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wake inalingana thamani halisi ya fedha inayotolewa (Value for money).
Mara baada ya kuapishwa mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdallah Hamisi Ulega alieleza kuwa kwa nafasi yake atatekeleza vema maamuzi ya vikao vya serikali na kusimamia hasa maamuzi ya Kamati ya Ushauri mkoa (RCC)kuhusiana na ununuzi wa zao la ufuta linalozalishwa kwa wingi wilayani kwake.Nae mkuu wa wilaya ya Nachingwea Regina Reginal Chonjo,Licha ya kushukuru kwa kuteuliwa Mkuu wa wilaya hiyo alihaidi kushirikiana na wananchi wa wilaya hiyo ambao tayari wamemwonyesha njia baada ya wananchi hao kujitolea kujenga jingo la ofisi ya mkuu wa wilaya na Halmashauri yao.Wakuu walioapishwa ni Dkt, Nassoro Ally Hamidi,aliyepangiwa wilaya ya Lindi, Abdallah Hamisi Ulega (DC,Kilwa),Regina Reginal Chonjo (DC Nachingwea),Agnes Elias Hokororo (DC Ruangwa) na Ephem Mbigi Mmbaga (DC Liwale). 
Picha na Habari toka kwa mdau Abdulaziz Video -Lindi0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa