Home » » MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA CHUO CHA UFUNDI STADI CHA VETA MKOA WA LINDI

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA CHUO CHA UFUNDI STADI CHA VETA MKOA WA LINDI



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal na Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim, wakikata utepe kwa pamoja kuashiria
uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Mkoa wa Lindi.
Uzinduzi huo ulifanyika jana Aprili 10, 2012. Kulia ni Mkurugenzi wa VETA, Zebadia Moshi.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA baada ya
kuzindua rasmi chuo hicho kilichojengwa Mkoa wa Lindi. Uzinduzi huo ulifanyika jana Aprili
10, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akibonyeza 'Alam', kuashiria uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA
kilichojengwa Mkoa wa Lindi. Uzinduzi huo ulifanyika jana Aprili 10, 2012. Picha na
Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa, Balozi wa
Korea nchini, Young-Hoon Kim na Viongozi wa VETA, wakati akitembelea na kukagua baadhi ya
majengo mapya yaliyojengwa ya Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA, baada ya kuzindua rasmi chuo
hicho mkoa wa Lindi jana Aprili 10, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Ghariub Bilal,
akisikiliza maelezo kuhusu jinsi ya ufundishaji wanafunzi kwa kutumia mtambo wa kufua
Umeme, kutoka kwa Mwalimu wa Umeme Veta, Majolo Mwigole, wakati Makamu alipofika kuzindua
Chuo hicho cha VETA mkoa wa Lindi jana Aprili, 10, 2012. 
Picha na Muhidin Sufiani-OMR


0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa