Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipata
maelezo kutoka Mtaalam wa Kutathimini mafunzo wa VETA Joyce Mwinuka
juu ya VETA inavyofanya kazi katika kuwajenga vijana katika mafunzo ya
elimu ya ufundi stadi katika maonesho ya Nanenane katika viwanja vya
Ngongo mkoani Lindi.
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipata
maelezo kutoka kwa Meneja uhusiano wa VETA, Sitta Peter wakati mkuu wa
JKT alipotembelea maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani
Lindi.
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipata
maelezo wa tofari ambazo zinaokoa gharama kutokana mazingira ambayo
kila mwananchi anaweza kumudu wakati mkuu wa JKT alipotembelea maonesho
ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Shamba darasa la JKT ndani maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Na Chalila Kibuda, Lindi.
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo
ameiomba Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kubuni
mpango maalum wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wanaoingia katika
mafunzo ya JKT ili wakitoka katika makambi waweze kupata fursa za ajira
katika maeneo mbalimbali.
Meja
Isamuhyo alitoa ombi hilo Jumatatu, Agosti 7, 2017 alipotembelea kwenye
banda la VETA, katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye
uwanja wa Ngongo, mkoani Lindi.
Alisema
vijana wanapoingia katika makambi ya JKT hupata mafunzo ya uzalendo na
ukakamavu kwa kipindi cha takribani miezi mitatu na kisha kuingia katika
mafunzo ya stadi za maisha na stadi za kazi kwa kipindi kipatacho
miezi 18.
Alifafanua
kutokana na mgawanyiko huo wa mafunzo ya JKT, VETA kwa kushirikiana na
jeshi hilo wanaweza kuweka mpango maalum wa kutumia kipindi cha miezi 18
ya mafunzo ya stadi za kazi na stadi za maisha kuandaa mafunzo ya
ufundi stadi ili kuwapatia vijana ujuzi utakaowawezesha kuajirika baada
ya kuhitimu JKT.
Alisema
JKT wamekuwa wakitoa mafunzo ya ufundi stadi mbalimbali, lakini
changamoto imekuwa ni kukidhi vigezo vya kutunuku vyeti vinavyotambulika
na VETA, kwani kipindi cha miezi minane ni kifupi katika kukidhi
matakwa ya mitaala ya VETA.
Alisema
kutokana na vijana hao kushindwa kupata vyeti vinavyotambulika na VETA
ambayo ni mamlaka ya kitaifa inayodhibiti na kusimamia mafunzo ya ufundi
stadi, inakuwa vigumu kwao kukubalika katika ajira au kujiendeleza
katika maeneo mbalimbali ya stadi walizozipata.
Alishauri
kuwa, kama mazungumzo na mipango mizuri itawekwa na VETA kwa
ushirikiano na JKT, kipindi hicho cha miezi 18 ya mafunzo ya JKT
kinaweza kupangwa vyema katika namna ambayo vijana watatimiza masaa
yanayohitajika kufuzu mafunzo ya ufundi stadi katika ngazi husika, hivyo
kutunukiwa vyeti vinavyotambulika na VETA.
Akijibu
juu ya suala hilo, Meneja Uhusiano wa VETA, Sitta Peter alimshukuru
Mkuu wa JKT huyo kwa ushauri na mawazo mazuri na kuahidi kuyafikisha
katika Menejimenti ya VETA kwa majadiliano na utekelezaji.
Alikiri
kuwa ni kweli kundi hilo la vijana wanaoingia katika mafunzo ya JKT ni
nguvukazi muhimu ikiwa wataandaliwa vyema katika mafunzo ya ufundi stadi
baada ya mafunzo ya ukakamavu na uzalendo yanayotolewa na JKT.
0 comments:
Post a Comment