Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Afisa
Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bw. Deodatus Alexander
akimkabidhi kitambulisho chake Bw. Abrahman Mohamed Mussa, akiwa
miongoni mwa wananchi waliokamilisha taratibu za Usajili na kukabidhiwa
Vitambulisho vyao wakati wa maonyesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye
viwanja vya Ngongo Lindi.
Baadhi
ya wananchi wakikamilisha taratibu za Usajili kwa kuchukuliwa alama za
vidole, picha na saini ya Kielektroniki wakati wa maonyesho
yanayoendelea Viwanja vya Ngongo Lindi.
Wananchi
wa Manispaa ya Lindi wakipata maelezo ya taratibu za Usajili toka kwa
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi.Rose Mdami wakati maonyesho ya
Nanenane yakiendelea mkoani Lindi.
Wananchi wakiendelea kusubiria kupata huduma ya Usajili kwenye banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) mkoani Lindi.
Bi
Khadija Khalid mtaalamu wa mifumo ya Komputa mkoani ofisi ya NIDA
Lindi, akitoa elimu kuhusu mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Taifa kwa
wananchi waliofika kujifunza kwenye Banda la NIDA.
Katibu Tawala wa Mkoa wa
Lindi Bw.Ramadhani Kaswa, ameipongeza na kuishukuru Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa NIDA kwa huduma nzuri kwa wananchi wa Lindi na mkoa jirani wa Mtwara
ambao wameendelea kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa katika siku za maonyesho ya
Nanenane Kitaifa yanayofanyika kwa mara ya nne mfululizo mkoani humo.
Mbali na kupongeza kazi
kubwa inayofanywa na NIDA, Katibu Tawala huyo amewahimiza wananchi kujitokeza
kwa wingi kusajiliwa kwani ni fursa muhimu ya kupata Vitambulisho vya Taifa kwa
wakati.
“ Wananchi jitokezeni kwa
wingi ili msajiliwe; hii ni fursa muhimu kwenu. NIDA hongereni sana na naomba
muendelee na ari hiyo ya kuwahudumia
wananchi” alisisitiza
Mamia ya wananchi wamejitokeza
kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa katika Maonesho ya Kilimo ya
Nanenane Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, sambamba
na kujifunza ukulima wa kisasa.
Wananchi mbali na
kusajiliwa; huduma nyingine zinazotolewa kwenye banda la NIDA; ni Ugawaji wa
Vitambulisho kwa wananchi waliokamilisha taratibu za Usajili, kutoa taarifa za
hatua ya uzalishaji Vitambulisho kwa wananchi ambao walishasajiliwa awali na
hawajapata Vitambulisho vyao, pamoja na kupata elimu ya jumla kuhusu
Vitambulisho vya Taifa, faida na matumizi.
Kupia fursa hii wananchi wanaosajiliwa
wameahidiwa kupata Vitambulisho vyao ndani ya mwezi mmoja ili kutoa fursa ya
uhakiki wa taarifa na uzalishaji.
0 comments:
Post a Comment