Home » » MWANDISHI WA HABARI MARIAM MKUMBARU AFARIKI DUNIA, KWA AJALI YA GARI

MWANDISHI WA HABARI MARIAM MKUMBARU AFARIKI DUNIA, KWA AJALI YA GARI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mwandishi wa habari, Mariam Mkubaru amefariki dunia.
Mkubaru alifikwa na umauti katika ajali ya gari inayodaiwa kutokea jana Ruangwa, mkoani Lindi akiwa katika shughuli zake.

Simu yake ilipojaribu kupigwa ili kupata ukweli wa tukio hilo, ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mama yake ambaye hata hivyo alishindwa kuzungumza kutokana na kulia.

Mkumbaru, amewahi fanyia kazi katika vyombo vya habari vya The Guardian Ltd, New Habari, Uhuru, Mzalendo, BBC, na baadae kuandikia mitandao ya kijamii Blogs.

Hadi anafikwa na umauti, alikuwa ni Mshauri wa Mradi wa Mama Yee unaotekelezwa na UTPC kupitia gazeti la Tuwasiliane.

Kifo hicho ni pigo lingine kwa tasnia ya Habari nchini Tanzania kufuatia mfululizo wa vifo vya waandishi vilivyotokea kwa mwaka huu ambapo vinadaiwa kufikia waandishi 7. 

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa