Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias 
Chikawe (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo mabati 2000 
kwa ajili ya ujenzi wa Maabara za Shule 20 za Sekondari wilayani humo. Waziri Chikawe 
ametoa msaada huo baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa agizo kwa kila mwana jamii nchini 
kuchangia ujenzi wa maabara katika shule za Kata nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias 
Chikawe (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo, Mwenyekiti wa 
Halmashauri ya Wilaya hiyo, Abdalla Chikawe (wapili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa 
Halmashauri ya Wilaya hiyo, Valery Kwembe wakiyaangalia msaada wa mabati yaliyotolewa na 
Mbunge wa Jimbo hilo kwa ajili ya kuzisaidia Shule za Sekondari za Kata kwa ajili ya ujenzi wa 
maabara. Makabidhiano ya mabati hayo 2000 yalifanyika nyumbani kwa Waziri Chikawe mjini 
Nachingwea leo. Picha zote na Felix Mwagara.
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment