.
 Mke
 wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM kwa mwanachama mpya 
wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Asha Chadenje aliyehama kutoka Chama Cha 
Wananchi,CUF wakati wa sherehe za uzinduzi wa sherehe za kutimiza miaka 
37 ya chama hicho zilizofanyika kimkoa huko Kiwalala, wilayani Lindi 
Vijijini tarehe 1.2.2013.
 Furaha ya kadi ya CCM
 Mke
 wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Salma Kikwete 
akimpongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama Cha Demokrasia na 
Maendeleo, CHADEMA, Mkoa wa Lindi Bwana Ali Omar Chitanda, ambaye 
amekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi. Mama Salma 
baada ya kumpongeza alimtambulisha kwa wananchi akiwa pamoja na Bi. Asha
 Chadenje wakati wa sherehe za uzinduzi wa miaka y37 ya CCM mkoani Lindi
 tarehe 1.2.2014.
 Mwenyekiti
 wa Chama Cha Mapinduzi, Mkoa wa Lindi Ndugu  Ali Mtopa akitoa hotuba 
fupi ya kumkaribisha Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ili aweze kuzindua 
rasmi sherehe za kutimiza miaka 37 ya CCM kwa Mkoa wa Lindi kwenye Kata 
ya Kiwalala huko Lindi Vijijini tarehe 1.2.2014.
IMG 
5076, 5119, 5189  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mamia ya 
wanachama wa CCM na wananchi wa Lindi Vijijini wakati akizindua rasmi 
sherehe za kutimiza miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi katika mkoa wa 
Lindi. Shughuli hiyo ilifanyika katika kata ya Kiwalala iliyoko Lindi 
Vijijini. Sherehe hiyo ilienda sambamba na kumnadi mgombea wa udiwani 
kupitia Chama Cha Mapinduzi  katika kata hiyo Bwana Shineni Hamis Zahoro
 katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 9.2.2014.
 Mke
 wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi 
anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akimnadi Mgombea
 wa Udiwani wa Kata ya Kiwalala kupitia CCM, Bwana Shineni Hamis Zahoro 
wakati wa sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika 
kimkoa katika kijiji cha Kiwalala terehe 1.2.2014.
 Baadhi ya wananchi katika sherehe hizo
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Mkoa wa Lindi Bwana Ali Omar Chitanda,
 Mke
 wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi 
anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akimnadi Mgombea
 wa Udiwani wa Kata ya Kiwalala kupitia CCM, Bwana Shineni Hamis Zahoro 
wakati wa sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika 
kimkoa katika kijiji cha Kiwalala terehe 1.2.2014.
 Mgombea
 wa Udiwani wa Kata ya Kiwalala kupitia CCM, Bwana Shineni Hamis Zahoro 
wakati wa sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika 
kimkoa katika kijiji cha Kiwalala terehe 1.2.2014.
 Mama Kikwete akimwaga sera za CCM
 Kicheko
 Ngoma
 ya Tambiko inayochezwa na wananchi wa kabila la wamakonde nayo ilikuwa 
ni kivutio tosha wakati wa sherehe za uzinduzi wa miaka 37 ya Chama Cha 
Mapinduzi zilizofanyika kimkoa  kwenye kata ya Kiwalala, Lindi Vijijini 

 wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ,Mama Salma
 Kikwete akiteta jambo na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi  Mkoa wa Lindi 
Dr.Maua Daftari (katikati) huku Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Lindi 
Vijijini akisikiliza wakati wa uzinduzi rasmi wa kumbukumbu ya kutimiza 
miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi zilizofanyika katika Kata 
ya Kiwalala iliyoko Lindi Vijijini tarehe 1.2.2014.
--------------------------
Mama Kikwete awataka wakazi wa wilaya ya Ruangwa kutunza ardhi yao na siyo kuiuza kwa wageni
Mke
 wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani
 Lindi kuitunza ardhi  nzuri na ya rutuba waliyonayo na kutokubali 
kuiuza  kwa wageni bali waitumie katika kilimo kwa kufanya hivyo 
watajipatia chakula cha kutosha na hivyo kuepukana na tabia ya kuomba 
chakula.
Mama
 Kikwete ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa aliutoa wito huo 
jana wakati wa kilele za sherehe za kutimiza miaka 37 ya  Chama Cha 
Mapinduzi (CCM) zilizofanyika katika kata ya  Likunja wilayani humo.
Mjumbe
 huyo wa NEC alisema wilaya hiyo imejaliwa kuwa na ardhi nzuri na rutuba
 ambayo mazao mengi yanastawi kwa wingi kama wananchi hao watumia ardhi 
hiyo kulima mazao ya vyakula kwa wingi wataepukana na tatizo  la njaa.
“Ardhi
 ni mali na ikitunzwa vizuri itawatunza hapo baadaye itumieni kulima 
mazao ya chakula kama mahindi, mihogo na mtu aone aibu kwenda kuomba 
chakula kwa jirani kwani hata watoto wenu wakila chakula kizuri na 
kushiba wataweza kuwa na afya njema na kusoma vizuri wawapo shuleni”, 
alisema Mama Kikwete.
Akizungumzia
 kuhusu CCM kutimiza miaka 37 Mjumbe huyo wa NEC aliwataka wakazi wa 
mkoa wa Lindi kutembea kifua mbele  na kujivuna kwani Serikali ya chama 
chao imefanya mambo mengi ya maana ikiwa ni pamoja na ujenzi wa 
barabara, shule, hospitali na kuboresha hali ya maisha ya wananchi wake 
ukilinganisha na miaka ya nyuma.
“Leo
 hii kuna baadhi ya watu wanapita na kusema kuwa Serikali haijafanya 
jambo la maana kitu ambacho si kweli kwani ukilinganisha  na miaka ya 
nyuma hivi sasa watoto wetu wanaomaliza darasa la saba wanajiunga na 
elimu ya Sekondari kwa wingi kwani shule zipo.  
Hivi
 sasa barabara ni nzuri na ni rahisi kwa mtu kusafiri kutoka  eneo moja 
hadi lingine tofauti na miaka ya nyuma  pia huduma ya afya imeimarika. 
Nawaomba  msiwe wanyonge tembeeni kifua mbele na pale mpakapoulizwa 
jibuni hoja kwani majibu mnayo”, alisema Mama Kikwete.
Mama
 Kikwete pia aliwataka wananchi hao kutunza amani, upendo na 
mshikamano  uliopo ili waweze kufika mbali kimaendeleo kwani vitu hivyo 
wakivipoteza ni sawa na kupoteza lulu waliyonayo.
 Amani
 ikitoweka hakuna jambo lolote litakalofanyika zaidi ya watu kukimbia 
huku na kule kunusuru roho zao, nchi zisizo na amani watu hawawezi 
kukusanyika kwa pamoja na kufanya mambo yao pamoja na demokrasia iliyopo
 nawashauri mjitahidi kuchagua vitu ambavyo vina maslahi ya Taifa.
Alisema,
 “Hao wanaowashawishi ninyi mfanye vurugu mbona kwao kuna aman?, ni 
ukweli kuwa mikoa ya Kusini ilikuwa nyuma kimaendeleo lakini sasa neema 
imepatikana baada ya kuendelea mnataka kurudi nyuma jitahidini kuwa 
wazalendo  na kutengeneza mazingira ya kujali kwenu kwa kufanya shughuli
 za maendeleo angalieni  msiwe chanzo cha matatizo katika maeneo 
mnayotoka”.
Kwa
 upande wake Mlezi wa Chama hicho katika mkoa wa Lindi Dk. Maua Daftari 
aliwapongeza wanachama hao kwa kuweza kutekeleza ilani yao ambayo 
imeweza kuwasaidia kufika miaka 37 na kusema kuwa wasisikitike na maneno
 ya kashfa yanayotolewa na wapinzani kwani ndiyo siasa ya vyama vingi 
ilivyo nao kama vyama vingine wamepata mdomo wa kusemea.
“Serikali
 iliamua kuanzisha mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ingawa katika kura 
zilizopigwa na wananchi  asilimia 80 walikataa na asilimi 20 ya wananchi
 walikubali lakini ilifanyika hivi ili wananchi wengine waweze wafanye 
kazi kwa pamoja na Serikali kupitia vyama vyao vya siasa na hii ndiyo 
demokrasia ya kweli”, alisema Dk. Daftari. 
Naye
 Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mzee Ali Mtopa aliwataka wapinzani waache
 tabia ya kukichafua chama hicho bali wakubali kuwa Serikali imefanya 
mambo mengi ya maendeleo na siyo kutukana viongozi waliopo madarakani 
bali kila mtu amwage sera za chama chake na siyo kashfa. 
Wakati
 huohuo  Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya
 Ruangwa  Saidi  Nng’umbanga  ambaye alialikwa katika sherehe hizo 
aliipongeza CCM kwa kufikisha miaka 37 na kuwa chama cha Demokrasia kwa 
kuvishirikisha vyama vingine vya siasa katika mambo mbalimbali.
Nng’umbanga
 alisema mikusanyiko ya wana Lindi na Mtwara ni ishara kuwa katika mikoa
 hiyo kuna amani ya kutosha na hakuna uhasama miongoni mwa watu kwani 
wanakutana katika mambo mbalimbali ikiwemo sherehe, misiba na mikutano 
ya siasa . 
Jumla
 ya wanachama waliojiunga katika wiki ya kilele cha sherehe hizo ni 1534
 kati ya hao kutoka chama cha upinzani cha CHADEMA ni 29 na Civic United
 Front (CUF) 21 
pia Chama hicho kimefanikiwa kuongeza idadi ya ofisi za kata hadi 
kufikia 142, matawi 1120 na mashina 11100 lengo likiwa ni kusogeza 
huduma karibu na wananchi.
 Mke
 wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa Chama Cha 
Mapinduzi Mkoa wa Lindi, Ndugu Ali Mtopa mara tu baada ya kuwasili 
kwenye Kata ya Likunja iliyoko katika wilaya ya Ruangwa ambako 
zilifanyika sherehe za miaka 37 ya CCM Kimkoa ambapo Mama Salma alikuwa 
mgeni rasmi tarehe 2.2.2014.
 Mke
 wa Rais Mama Salma Kikwete akielekezwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi
 wa Mkoa wa Lindi,Ndugu Adeline Gefi sehemu ya kupita ili kupokea 
maandamano ya wana CCM na wananchi wa mkoa huo wakati wa kilele cha 
sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa chama hicho zilizofanyika katika Kata ya
 Likunja, wilayani Ruangwa tarehe 2.2.2014. Wa kwanza kulia ni Dr. Maua 
Daftari, Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Lindi.
 Mke
 wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Mama Salma
 Kikwete akiwapungia wananchi waliofika kwenye sherehe za kilele za CCM 
kutimiza miaka 37 zilizofanyika kimkoa katika Kata ya Likunja, wilayani 
Ruangwa tarehe 2.2.2013
 Mke
 wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma 
Kikwete akipokea maandamano ya wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Lindi 
wakati wa sherehe za kilele cha kutimiza miaka 37 ya Chama Cha 
Mapinduzi  mkoani humo zilizofanyika katika kata ya Likunja iliyoko 
katika wilaya ya Ruangwa tarehe 2.2.2014.

 wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua shina la wakereketwa la Jumuia ya 
Wanawake Tanzania (UWT) katika Kata ya Likunja wakati wa kilele ya 
sherehe ya miaka 37 ya CCM zilizofanyika katika kata hiyo tarehe 
2.2.2014. Mara baada ya kuzindua tawi hilo Mama Salma akapokea shada la 
maua kutoka kwa mmoja wa viongozi wa UWT wa Kata hiyo na picha ya mwisho
 ikiwaonyesha akina mama wajumbe wa Tawi hilo wakishangilia baada ya 
uzinduzi huo.
 Mke
 wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka Bibi Mwanahawa Ali, 
mjumbe wa UWT wa Kata ya Likunja kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya 
Ruangwa wakati wa kilele cha sherehe za CCM kutimiza miaka 37.
 Ngoma
 za utamaduni  za makabila mbalimbali ya mkoa wa Lindi zilishamiri 
katika kilele cha sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi 
zilizofanyika  Mkoani Lindi katika Kata ya Likunja huko wilayani 
Ruangwa. Hata muziki wa kizazi kipya nao uliporomoshwa katika kilele 
hicho.  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alikuwa Mgeni Rasmi kwenye 
sherehe hizo

  Mgeni
 Rasmi katika sherehe za CCM kutimiza miaka 37 katika Mkoa wa Lindi, 
Mama Salma Kikwete akikata keki maalum ya sherehe na kuwalisha wana CCM 
waliozaliwa mwaka 1977, ambapo Chama Cha Mapinduzi kilizaliwa.
 Mmoja wa wana CCM akilishwa keki
 Mgeni
 Rasmi katika kilele cha sherehe ya kutimiza miaka 37 ya Chama Cha 
Mapinduzi, Mkoani Lindi, Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wana 
CCM na wananchi wa Mkoa wa Lindi katika sherehe zilizofanyika katika 
Kata ya Likunja, wilayani Ruangwa  tarehe 2.2.2014.

 Baadhi
 ya wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Lindi wakisikiliza hotuba ya mgeni 
rasmi, Mama Salma Kikwete wakati wa kilele cha sherehe za kutimiza miaka
 37 ya chama hicho zilizofanyika katika kata ya Likunja, wilayani 
Ruangwa tarehe 2.2.2014.

Ruangwa tarehe 2.2.2014. Picha zote na John Lukuwi
 
0 comments:
Post a Comment