Home » » WILAYA YA KILWA LINDI, WAANZA KUNUFAIKA NA GESI ASILIA

WILAYA YA KILWA LINDI, WAANZA KUNUFAIKA NA GESI ASILIA


Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akishuhudia utiaji wa sahihi
wa mkataba huo wa miaka mitatu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Addo Mapunda
akitiliana saini na  Bi Anne Devilliers,Mratibu wa Mradi wa mpango wa
ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa
(Techonoroji Enhanced Edcation) TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya
Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji
na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo
Na  Abdulaziz Video mwandishi  wa www.francisgodwin,blogspot.com ,Lindi

WANAFUNZI wapatao 1,580 wanaosoma Shule tisa za Sekondari,wilayani
Kilwa, mkoani Lindi,watanufaika na mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya
Kingereza kwa njia ya teknolojia ya kisasa TEE-TZ chini ya ufadhili wa
kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya
uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.

Mradi huo wa miaka mitatu,utagharimu jumla ya Sh, ya
Sh,144,945,218/-zitakazotumika kujenga misingi bora ya Lugha ya
kingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia  mwaka 2013.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo,
Adoh Mapunda,alipokuwa akitoa taarifa katika hafla fupi ya kutiliana
na saini ya utekelezaji wa mpango huo.

Mapunda alisema mpango huo,utakaochukuwa takribani muda wa kipindi cha
miaka mitatu,umeanza rasmi mwezi  huu kwa wanafunzi wapatao 1,580 wa
kidato cha kwanza kutoka Shule tisa za Sekondari zilizopo katika
wilaya hiyo.

Amezitaja Sekondari zitakazonufaika na mpango huo kuwa ni,Kilwa day
iliyopo mji mdogo wa masoko, Mtanga, Songosongo, Mbuyuni,
Kinjumbi,Miteja,Mingumbi,Kikanda na Sekondari ya wasichana ya Ilulu.

Mkurugenzi Mapunda alisema mafunzo hayo kwa kuanzia yatakuwa ni ya
wiki sita,yameanza rasmi hivi karibuni na kwamba walimu wapatao 30
wakiwemo (12) wa kigeni (Volunteers) wakiwemo na walimu wazawa (18).

“Hizi Shule tisa kila moja italazimika kutoa walimu wawili
watakaopatiwa mafunzo kwa ajili ya kuendesha mpango huu katika Shule
zote hizo”Alisema Mapunda.

Aidha, Mapunda alisema kupitia ufadhili wa mpango huo wa mafunzo ya
kingereza,Halmashauri ya wilaya itaendesha semina/warsha kutoa stadi
za kufundishia masomo hayo kwa Sekondari hizo tisa zenye walimu
wapatao (71).

Mapunda alisema mafunzo hayo ni nyongeza kwa walimu wote waliopo
katika Shule hizo tisa za mafunzo ya kingereza ya aina mbili,TEE-TZ
itakayoendeshwa kwa ufadhili wa ubalozi wa Marekani,(RELO-Regional
English Language Office kwa Sh,24,158,480/-.

Katika ufadhili wa mafunzo hayo ya TEE-TZ na RELO jumla ya
Sh,169,103,698/-ndizo zitakazotumika kwa ajili ya utekelezaji wake.

Mratibu wa mradi huo,kutoka kampuni hiyo ya Pan African Energy,Anne
Devilliers,amesema lengo la mpango huo ni,kutaka kuwawezesha wanafunzi
waelewe masomo yao kwa elimu ya Sekondari na kuongeza viwango vya
ufaulu katika mitihani yao ya kidato cha nne.

Devilliers akasema imebainika kwamba wapo wanafunzi waliowengi
wamekuwa hawafanyi vizuri katika masomo na mitihani yao,kutokana na
kutoielewa vyema Lugha ya Kingereza.

Mkuu wa wilaya hiyo ya Kilwa, Abdallah Ulega, ameipongeza kampuni ya
Pan African Energy,na akasema kwamba kwa kiasi furani itasaidia
kuboresha kiwango cha elimu ndani ya wilaya hiyo,mkoa na Taifa kwa
ujumla.

Mpango huo,ulianza kwa majaribio katika wilaya ya Mafia mkoani
Pwani,mwaka 2010 na 2011,baada ya kuona mafanikio yake,ndipo uongozi
wa wilaya ya Kilwa,ukaamua mpango huo kupelekwa ndani ya wilaya yao.
Mwisho.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa