Na Bashir Yakub.
Tumegusa
uchumi wa bepari. Mara zote, na kote duniani bepari alipoguswa kwenye
uchumi wake basi ametumia mbinu hizi hapa chini kuhakikisha anapambana
na waliomzuia.
[a]
Kumwita kiongozi anayeongoza vita ya uchumi Mvunjaji wa haki za binadamu
na asiyefaa. Imetokea kwa Gaddafi baada ya kumnyima bepari mafuta,
halikadhalika kwa Saddam Hussein.Pia ndilo tatizo la Mugabe na bepari baada ya kurudisha mashamba kwa wazawa ili wafaidi uchumi wao.
[b] Kuratibu na kufanikisha matukio ya ajabu kwenye jamii ili kuleta faraka,taharuki, chuki, uadui, na sintofahamu.Bepari analiweza sana hili hasa nchi za Afrika kutokana na uwezo wake mkubwa wa fedha na teknolojia.
Lengo la mbinu hii ni :
Mosi,kuwatoa kwenye ajenda ya vita dhidi yake na kuwaelekeza kwenye mijadala mingine.
Pili, kuchonganisha watu, serikali na viongozi wao.
Tatu, kupeleka ujumbe duniani kuwa kiongozi fulani na serikali yake hawafai tena.
Nne, kuligawa taifa kati ya upande unaoamini matukio kutekelezwa na fulani na upande unaoamini vingine.
[c] Kuandaa mapinduzi kwa kuwatumia wasaidizi wa rais na viongozi wenye tamaa.
[d] Kuandaa maandamamo makubwa ambayo mwisho wake ni kuuondoa utawala uliodhibiti uchumi .
Utaona waandamanaji wanalalamika kuchoshwa na mambo mbalimbali lakini nyuma yao ni fedha, mbinu na mipango ya bepari.
Bila
hata waandamanaji kujua isipokuwa wachache/viongozi wao. Mbinu hii
imetumika hivi karibuni kuondoa viongozi wengi wa Afrika ya Kaskazini
waliodhibiti uchumi wao kwa mda mrefu.
[e]
Kufadhili makundi ya waasi Mf. Congo, Sudani Kusini, Sierra Leone,
Liberia nk. Mnajua kuwa hadi baadhi ya makundi ya kigaidi hufadhiliwa na
hawa jamaa.
Badala ya kujadili udhibiti wa rasilimali zenu mnajadili amani itapatikana vipi huku bepari akitumia nafasi hiyo kuiba.
[f]
Kufadhili na kuviimarisha vyama vya upinzani hasa vyenye tamaa ili
hatimaye na kwa namna yoyote ile viondoe madarakani viongozi waliombana
bepari.
[g]
Kutafuta sababu na hatimaye kuweka vikwazo vya kiuchumi kwa nchi husika
ili kulainisha au kumaliza kabisa misimamo ya serikali na viongozi dhidi
ya rasirimali anazozitaka bepari.
Pia
lengo ni kuwafanya wananchi wapate taabu ili wachoshwe na utawala
uliombana bepari na hivyo kufanya maamuzi ya kuuondoa kwa namna yoyote.
nk, nk, nk............
NINI MFANYE KTK KIPINDI KAMA HIKI.
[a] Kushikamana na kutokubali kutenganishwa kwa matukio.
[b]Kutokuwa na majibu ya haraka katika mambo makubwa.
[c]
Vyombo vya usalama kujiimarisha kiulinzi na kuhakikisha vinafika kwenye
majibu ya mzizi wa kila tukio na kutoa taarifa kwa wakati kwa umma.
[d]
Vyombo vya usalama kutokubali kusaidiwa upelelezi na nchi za mabepari
kwakuwa mwanya huo hutumika kutoa majawabu aidha yanayokwepesha(divert)
ukweli au yanayokamilisha malengo yaliyokusudiwa.
[e] Kuepuka kabisa kuchanganya tofauti zetu za kisiasa za tokea huko nyuma na yanayotokea sasa.
YAPI MADHARA YA KUTOSHIKAMANA KIPINDI KAMA HIKI.
Bepari
hana hasara, wenye hasara ni mimi na wewe. Mpango wa wagawe uwatawale
"divide&rule" haikuishia kwenye ukoloni. Bado ungalipo.
Kama
tutakubali kugawanywa na majaribu ya bepari , sawa na tugawanywe tu ,
ila ahadi ni hii kuwa kila mmoja ataonja joto la jiwe.
Wewe
uliyekubali kugawanywa utaonja na ambaye hakukubali ataonja. Mtaona Iraq
na Libya aliyeshiriki na ambaye hakushiriki wote wanaonja.
Hakuna
atakayekuzuia kukomaa na msimamo wako. Hakuna atakayekuzuia kuamini
mbowe ndiye aliyefanya tukio fulani ili kumzuia fulani kugombea
uenyekiti. Hakuna atakayekuzuia kuamini kuwa Lowassa ndiye aliyefanya
tukio fulani ili kumzuia fulani kugombea urais 2020. Lakini pia hakuna
atakayekuzuia kuamini kuwa serikali ndiyo iliyofanya tukio fulani
kwasababu yule au ofisi ile kuna wabaya au wakosoaji wake.
Wewe
amini hivyohivyo unavyoamini ila kaa ukijua kuwa ikiwa tutagawanyika tu,
basi kila mtu, kila familia, kila kundi, kila chama, na imani yako
hiyohiyo uliyonayo yatakufika. Madhara ya bepari yanapokuja hayaangalii
nani alikuwa akiamini nini, ama nani alitumia gani tukio kumsema nani.
Mtaona
Libya kusini ina serikali yake, kaskazini ina serikali yake , magharibi
yake na mashariki yake.Ni vipandevipande, shida juu ya shida. Na humo
wamo wote walioshiriki na ambao hawakushiriki. Madhara ya bepari
hayaangalii aliyeshiriki na ambaye hakushiriki.
Kwahiyo
wewe msaidie tu bepari kwakujua au kutokujua kueneza propaganda zake
kwa matukio anayoyaandaa ila ujue kuwa mwisho wa tamthilia tutakuwa wote
tuu. Wala huna pa kwenda ndugu tutalia wote humuhumu.
Na
mkishakuwa nyang’anyang’a, bepari ameshawashinda, na hamna tena la
kumfanya, na sasa anawageuza anavyotaka, basi hapo bepari atakuja na
kusema ukweli kuwa si fulani aliyefanya tukio fulani bali ni sisi kwa
lengo fulani.
Mnakumbuka
wale walioiharibu Iraq baadae walisema ukweli. Waliandika vitabu kuwa
vita ile ilikuwa ya makosa na kule hakukuwa na silaha za sumu kabisa. Ni
baada ya kuiharibu vibaya sana nchi hiyo na kuiletea dhiki na mashaka
makubwa.
Mnakumbuka
walioiharibu Libya nao baadae walisema ukweli. Sasa wanasema wazi kuwa
makundi waliyoyatumia kumg’oa Gaddaffi hayakuwa makundi sahihi bali ya
imani kali.
Lakini
mwanzoni walikataa kuwa hawako nyuma ya makundi yaliyoanzisha
maandamano na kusema kuwa wananchi waliochoka udikteta wa Gaddaffi ndio
wanaoandamana. Bepari akishakumaliza anakiri. Basi kwa kiwango gani
mnakuwa mmedhalilika na kudharauliwa ndugu zangu. Ni lini wananchi wa
Afrika tutajifunza kutoka matukio haya.
Tunawalaumu
viongozi wetu waafrika lakini pia sisi wananchi wa Afrika kwa nafasi
zetu kama wananchi tunayo mambo ya kujifunza na kushughulikia lakini
hatufanyi hivyo. Ni lini basi tutaacha kudhalilishwa na bepari. Toka
ukoloni mpaka uhuru hatujifunzi tuu ndugu zangu. Basi tutajifunza lini ,
makaburini ama.
Tujihadhari
kwani kwetu tayari bepari ameanza kwa matukio ya hapa na pale.
Tukimuunga mkono kwa vinywa vyetu huku tukijua tunamkomoa kiongozi
fulani au chama fulani, basi atatuvuta taratibu taratibu mpaka huko
Libya na Iraq halafu yeye aendelee kuiba kama alivyokuwa amezoea awali.
Ndugu zangu, tunawasifia Angola na Botswana kwa kumbana bepari na hatimaye kufaidi rasimali zao sasa.
Lazima tujue wamefikia hapo baada ya kushikamana na kuzishinda hila, fisadi, fitna,na mitihani ya bepari. Na sisi tunaweza.
TUTARAJIE MATUKIO ZAIDI.
Matukio
bado , huu ni mwanzo tu. Hivi mlitarajia bepari abanwe halafu tubaki
salama. Haiwezekani. Historia inakataa jambo hilo. Bepari lazima
akutingishe.
Kama ingekuwa tumbane bepari halafu tubaki
salama
basi isingeitwa Vita ya Uchumi bali Sherehe ama tafrija ya Uchumi.
Yanini iitwe vita kama mmembana bepari na bado mkaendelea kuwa salama na
kufurahia maisha. Hii ni vita na sasa mnaweza kuanza kuona taswira ya
vita yenyewe.
Vitimbi na matukio yatakuja mengi. Lengo ni moja tu , kuua vita hii ili bepari aendeleze alikoishia.
Msishangae
wakaanza kudhuliwa hata wanaoonekana wana mtazamo tofauti na mwenyekiti
ndani ya chama tawala ili chama kigawanyike na hatimaye serikali
igawanyike. Bepari anajua ukigawa chama kinachotawala umeigawa serikali
kwakuwa wanachama wa chama tawala ndio huunda serikali.
Hivyo kwa kufanikiwa kukigawa chama kinachotawala bepari anajua atakuwa amefanikiwa kuigawa serikali.
Ukifanikiwa
kuigawa serikali maana yake bepari amepunguza kasi ya vita dhidi yake
lakini maana yake pia anakaribia kumwondoa kabisa adui aliyebana uchumi
wake.
Bepari
haoni tabu kumdhuru yeyote ama chochote ili kutimiza malengo yake.
Bepari anajua ukimdhuru kiongozi mwenye mawazo tofauti ndani ya chama
ama serikali , basi watanyoosheana vidole. Yule aliyedhuriwa atapata
kundi lake wanaoamini ameonewa na wale wengine watabaki kundi jingine.
Bepari anajua kuwa hata kiongozi awe mkali ama na msimamo kiasi gani
hawezi kusimama kama wasaidizi wake wamegawanyika.
Ni vita ya uchumi , na sasa tunaonja shubiri yake. Ila tutashinda.
MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MCHAMBUZI WA MASUALA YA SIASA. 0784482959.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment