Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula (Mb) akiongea jambo na Meneja wa PPF Kanda ya Kusini Bi Zaida Mahava (kushoto) pamoja na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF baada ya kupewa maelezo ya namna ya Mfumo wa WOTE SCHEME unavyofanya kazi na faida zake kwa sekta isiyo rasmi wakati alipotembelea Banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
Meneja wa PPF Kanda ya Kusini Bi Zaida Mahava akimuelekeza Mwananchi jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na mfumo wa hiari wa Wote scheme baada ya kupewa elimu alipofika katika Banda la PPF lililopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula (Mb) alipotembelea banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula (Mb) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema "
Wote scheme ni Mkombozi kwa wananchi wengi walio katika Sekta isiyo
rasmi na ameushahuri Mfuko wa Pensheni wa PPF kushirikiana na Maafisa
Maendeleo ya Jamii kupitia Ofisi za Halmashauri ili kuweza kuwafikia kwa
urahisi jamii ambayo haipo kwenye ajira rasmi na kuweza kunufaika na
Mfumo huo.
Mfuko
wa Pensheni wa PPF unashiriki katika Maonesho ya Nane nane kitaifa
Lindi kwa lengo la kuendelea kutoa elimu kwa wananchi hasa walio
katika sekta isiyo rasmi kama vile wakulima, wafugaji, Wavuvi,
wajasiriamali wakubwa na wadogo na wengine wote waliojiajiri wenyewe juu
ya Mfumo wa " Wote scheme " ambao unawawezesha kujiwekea akiba wakati
huo huo wakipata fursa za mafao ya Uzeeni, huduma za bima ya afya,
mikopo ya maendeleo na mikopo ya kujiendeleza kielimu.
Vilevile
kwa wale walioajiriwa wanaweza kumtumia Mfumo huu wa "Wote scheme"
kama mfumo wa hiari wa kujiwekea akiba Zaida Mahava, Meneja wa Mfuko
wa Pensheni wa PPF Kanda ya kusini amesema kwa kutambua kundi kubwa la
jamii ambalo halipo kwenye ajira rasmi wameona ipo haja ya kutoa elimu
juu Mfumo wa Wote scheme ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na
PPF kupitia Mfumo wa Wote scheme.
0 comments:
Post a Comment