Kaimu
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo (Kushoto) ambaye pia ni Mkuu
wa Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo ya Kilimo, Uvuvi
na Ufugaji mara baada ya kutembelea
banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane
katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Kaimu
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya
ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo ya Kilimo, Uvuvi na
Ufugaji mara baada ya kutembelea banda la
Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Nanenane katika
viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Kaimu
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya
ya Nanyumbu akiwasili katika banda la wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi
wakati wa Maonesho ya Nanenane katika
viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Kaimu
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo (Kushoto) ambaye pia ni Mkuu
wa Wilaya ya Nanyumbu akisikiliza kwa makini maelekezo kwa Mkurugenzi
wa Farm Base Ltd Ndg Suleiman Msellem
kuhusu Pembejeo za kilimo, na ushauri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji mara
baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa
Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi

Na Mathias Canal, Lindi
Wakulima,
wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla wameombwa kushiriki kwa wingi
katika Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane yanayofanyika kwa
siku 8 katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joachim Wangabo
ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu wakati akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho.
Mhe
Wangabo alisema kuwa Maonesho ya mifugo sanjari na Maonesho ya Kilimo
hutoa changamoto ya kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na
kutoa ajira hususani kwa vijana kuwaongezea zaidi kipato
na kuondoa umasikini hivyo wananchi kushiriki kwao kutawahakikishia
elimu mbadala ya kilimo chenye tija kwao na Taifa kwa ujumla.
Maonesho
hayo yanabebwa na kauli mbiu mahususi kwa mwaka huu 2017 isemayo
"Zalisha kwa Tija Mazao ya Bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia
Uchumi wa Kati" ikiwa imedhamiria kwa kiasi kikubwa kumkwamua
mwananchi na mkulima wa kawaida kuondokana na uduni wa mazao wakati wa
mavuno.
Katika
Maonesho hayo Wizara, taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na
wadau wote wa kilimo na mifugo wanatekeleza jukumu kubwa la kuwaelimisha
wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji
kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa
kuanzishwa.
Teknolojia/Bidhaa zinazooneshwa ni pamoja na zana za Kilimo, Mbegu bora za mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira yaliyodhibitiwa ambapo piaTaasisi za kitafiti ambazo zitaonyesha teknolojia mbalimbali za kuongeza tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa mbalimbali, Utengenezaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo, Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na mazao ya kilimo yanayostahimili hali ya hewa kutokana na maeneo walipo wananchi wanaohitaji kujihusisha na ufugaji na kilimo na udhibiti wa magonjwa.
Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, ambapo Taasisi za elimu zitaonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.
Hivyo kwa wingi wao wananchi waishio Kanda ya kusini katika mikoa ya Lindi na Mtwara wanapaswa kutumia fursa hii ambayo inatokea katika kipindi kimoja pekee katika kila mwaka.

Mhe Wangabo alisema kuwa Tatizo kubwa linalokabili sekta ya kilimo na ufugaji nchini kutozingatia kanuni bora na za kisasa za
kilimo na Ufugaji. Nimefurahishwa sana kuona kwamba katika maonyesho haya kuna Taasisi za utafiti zinazozalisha mbegu za kisasa.
Alisema
kuwa zipo changamoto zinazokabili sekta ya kilimo na mifugo nchini
ikiwa ni pamoja na ukame, upungufu wa madawa ya mifugo, uchache wa
maafisa mifugo,
upungufu wa majosho, uvuvi haramu na miundombinu duni ya kusafirisha
mazao ya mifugo.
0 comments:
Post a Comment