Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Anna Nkinda – Maelezo,
Lindi
Vijana wametakiwa
kutokubali kutumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa kwa maslahi ya watu wachache huku hao
wanaowatumia wanasonga mbele kimaendeleo na wao wanazidi kurudi nyuma.
Rai hiyo imetolewa jana
na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwa nyakati tofauti na
wananchi wa kijiji cha Kikomolela kilichopo
jimbo la Mchinga na mtaa wa Likotwa
uliopo Jimbo la Lindi mjini waliohudhuria kampeni ya kuwanadi wagombea wa
nafasi za udiwani, ubunge na urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mama Kikwete ambaye ni Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema kuna
baadhi ya wanasiasa wanawatumia vijana kufanya vurugu ambazo hazina faida katika jamii zaidi ya kuleta hasara kwani wanaharibu
miundombinu ikiwa ni pamoja na barabara, majengo na hivyo kurudisha maendeleo
nyuma.
Kuhusu uchaguzi aliwaomba
wananchi wote wa maeneo hayo wakiwemo wanachama wa vyama vya upinzani kuwachagua wagombea wa CCM ambao
watazidi kuwaletea maendeleo kwani
Serikali ya CCM imefanya mambo mengi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha
huduma za afya, elimu, maji na barabara.
“Siku ya uchaguzi
ikifika chukua kadi yako ya kupigia kura wahi mapema kituoni kachague viongozi
bora utakaoona watakuletea maendeleo na viongozi hawa wanapatikana ndani ya CCM.
Msiogope! siku hiyo kutakuwa na usalama
wa kutosha”, MNEC huyo alisisitiza.
Kwa upande wake mgombea
ubunge wa jimbo la Mchinga Saidi Mtanda alisema Serikali ya CCM imefanya mambo
mengi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma
ya umeme na katika eneo hilo vijiji 40 kati ya 47 vikiwemo vijiji vya Nangaru
na Kitomanga karibu vitawasha umeme kwa
gharama ya shilingi 45,000/=.
Mtanda alisema, “Nawaomba
wenzetu kutoka vyama vya upinzani dumisheni hali ya Amani na utulivu iliyopo kwani kuna
baadhi yenu mnatoa kauli za kuwatisha
wanachama wa CCM kitendo ambacho siyo kizuri”,.
Naye mgombea Ubunge wa
Jimbo la Lindi mjini Kaunje Selemani aliwaomba wananchi waliohudhuria mkutano
huo kumpigia kura ya ndiyo na kuwaahidi kusimamia Ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo itawaletea maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo za nishati na madini, kilimo, elimu, afya, maji, umeme
na barabara.
Katika mikutano hiyo
jumla ya wanachama watatu walihama kutoka chama cha Wananchi (CUF) na kujiunga na CCM.
Wakati huo huo akiwa njiani
kuelekea kijiji cha Kikomolela msafara wa Mama Kikwete ulisimama Shule ya
Msingi Moka ambapo walimu na wanafunzi walikuwa wamesimama pembeni ya barabara
wakiwa wameshika bango lililoandikwa SHULE YA MSINGI MOKA TUNAUJUMBE KWA MAMA
KIKWETE.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa
shule hiyo Abdala Mkanjima alimuomba Mama Kikwete ambaye kitaaluma ni Mwalimu awasaidie
kufanya wire ring katika shule yao kwani umeme umepita shuleni hapo.
Mama Kikwete aliahidi
kulishughulikia suala la umeme katika shule hiyo. Pia aliwaasa
wanafunzi wasome kwa bidii ili waweze kujikomboa kimaisha na kuwa viongozi wazuri hapo baadaye ambao
watalisaidia taifa lao na jamii
inayowazunguka.
0 comments:
Post a Comment