Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Meneja Kiongozi
wa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume(wa tatu Kushoto) akiwa na
Kaimu Meneja Mkoa wa Lindi, Jumbe Dona (wa pili Kushoto), Afisa
Matekelezo Kuruthum Yusufu ( Wa kwanza Kushoto), Afisa Mwandamizi wa
Uhusiano Salim Kimaro (wa tatu Kulia), Afisa Uendeshaji Muandamizi Abasi
Cothema (wa pili Kulia) na Afisa Mafao wa Mkoa wa Lindi Paschal Mushi
(Wa kwanza Kulia) kwenye mkutano wa Wadau wa Korosho unaofanyika leo
katika hoteli ya Peace Beach Mkoani Lindi.
Maofisa wa NSSF wakiwasaidia wadau wa Korosho kujaza fomu za uanachama ili waweze kujiadikisha kujiunga na NSSF.
Meneja
wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF), Mkoa wa Mtwara, Stanley
Milanzi akitoa mada kwa wadau wa zao la Korosho kwenye mkutano wa mwaka
wa wakulima wa korosho uliofanyika leo mkoani Lindi.
Meneja
Wa NSSF Mkoa wa Mtwara, Stanley Milanzi akiwaelekeza wadau wa Korosho
jinsi ya kujaza fomu za NSSF ili waweze kujiandikisha na NSSF.
Meneja
wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF), Mkoa wa Mtwara, Stanley
Milanzi akitoa mada kwa wadau wa zao la Korosho kwenye mkutano wa mwaka
wa wakulima wa korosho uliofanyika leo mkoani Lindi.
SHIRIKA
la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limeshiriki kwenye mkutano wa Wadau
wa Korosho unaofanyika kwenye Hoteli ya Peace Beach Mkoani Lindi,mkutano
huo utakaofanyika kwa Siku mbili mfululizo utahusisha wadau wa Korosho
kutoka Tanzania nzima.
Katika
Mkutano huo ambao NSSF imepata nafasi ya kutoa mada imewahimiza wadau
hao waweze kujiunga na NSSF ili waweze kupata mafao bora yatolewayo na
mfuko huo, Mafao hayo yakiwemo Matibabu bure, Kuumia Kazi, Uzazi kwa
Kina mama , Mikopo kwa wanachama na Mengineyo.
Akiongea
katika Mkutano huo Meneja wa NSSF Mkoa wa Mtwara , Stanley Milanzi
amewaambia wadau huo kupitia Mpango wa NSSF Wakulima Scheme wakulima wa
Mkoa wa Mtwara wamepata karibia Shilingi bilioni mbili kama mikopo
kutoka NSSF.
NA MICHUZI MEDIA GROUP
0 comments:
Post a Comment